powered by
send-it.me

Adventist World-Kiswahili inamshukuru kila aliyejiandikisha kwa ajili ya jarida hilo, kupitia kwa jukwaa letu la awali, yaani chaneli ya WhatsApp. Tumefurahia kupokea jumbe kutoka kwako, na vilevile shuhuda za jinsi umetumia jarida hili linalotia moyo kuwafikia wengine kwa ajili ya Kristo!

Tungependa ujue kuwa tulihamia jukwaa jipya tangu Februari 2024. Zaidi ya yote, tungependa uhame pamoja nasi. Adventist World-Kiswahili haitaki kumwacha nyuma yeyote aliyejiandikisha.

 

Badala ya kupokea ujumbe wa WhatsApp pamoja na toleo jipya kila mwezi, sasa tunakupa kiungo kwa tovuti ya bure ambayo ni nzuri kwa simu, ambapo unaweza kuyasoma makala yote, kama kawaida. 

Pia tutakiweka kiungo hicho kwenye ukurasa wa Facebook wa Adventist World-Kiswahili kila mwezi, ambapo unaweza kututumia jumbe na taarifa kuhusu jinsi makala hii inakufaidi wewe na jamii yako. Pia unaweza kututumia maoni na mapendekezo jinsi ya kuifanya makala hii iwafae zaidi wasomaji!

Ukipenda, unaweza kutuma baruapepe: 
kwambokaj@ecd.adventist.org ukiwa na maswali yoyote.

 

Moja ya manufaa ya tovuti mpya ya Adventist World-Kiswahili ambayo ni nzuri kwa simu, ni kwamba kutakuwa na lugha zingine nyingi za kuchagua, ikiwa ungependelea Kiingereza au lugha nyingine yoyote, unaweza kuangalia kama ipo, kando na ile ya kawaida ya Kiswahili.

 

Manufaa mengine ni kwamba ni rahisi kushiriki kiungo hicho kipya cha Adventist World-Kiswahili, kwa marafiki na familia. Tunakuhimiza ufanye hivyo. Hebu iangalie sasa hivi.

 

Tunatumai kuwa na uhusiano mrefu na wa furaha na wasomaji wetu wa Adventist World-Kiswahili.

 

Mungu akubariki,

 

Timu ya Adventist World-Kiswahili

Tunaamini katika nguvu ya maombi, na tunakaribisha hitaji la maombi ambayo tutashiriki katika ibada ya watendakazi kila Jumatano asubuhi. Tuma maombi yako kwa kwambokaj@ecd.adventist.org, na utuombee tunapofanya kazi pamoja kuendeleza ufalme wa Mungu.

 

Picha ya jalada: sezer66 / iStock / Getty Images Plus  / Getty Images 

Japokuwa ugonjwa tandavu wa UVIKO-19 ulianzisha chanjo za RNA ulimwenguni, matumizi ya tiba ya virusi na vinasaba yamekuwepo tangu karne iliyopita. Matibabu ya virusi ni nyenzo ya viini vya vinasaba vya virusi kubadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa na taarifa mpya za vinasaba vya matibabu. Kisha virusi visivyo na madhara vinaingizwa ndani ya mwili na nakala zake zisizo na madhara za DNA hurekebisha hali zozote zilizosababishwa na mabadiliko ya awali.

 

Utafiti mmoja ulihusisha tiba ya vinasaba kwa ugonjwa unaoitwa Leber congenital amaurosis (LCA). Ugonjwa wa LCA ni mojawapo ya sababu maarufu ya upofu wa kurithi wakati wa kuzaliwa. Kuna aina nyingi na udhihirisho tofauti wa LCA, lakini zote huathiri uwezo wa kuona.*

 

Kama ilivyo katika matibabu mengine mengi ya kuona, matokeo yalikuwa ya kuridhisha lakini yasiyohitimishwa. Sababu ilikuwa kwamba wakati jicho lenyewe linaweza kuwa limeponywa, ubongo ulikuwa bado hauwezi kuleta maana ya picha zinazoonekana. Kama upofu ungekuja baadaye maishani, ubongo ungejua ushughulike vipi na kuona kulikorejeshwa kwa sababu mtu huyo alikuwa akiona kabla. Wale vipofu tangu kuzaliwa wangehitaji, si macho mapya tu, bali njia mpya za mishipa ya fahamu.

 

Fikiria kuwa haujawahi kuona kitu hapo kabla, hakuna kumbukumbu, hakuna chochote; halafu ukaona. Ungejuaje kile ulichoona? Ukweli huu hufanya uponyaji wa kipofu wa Yohana 9 kuwa wa ajabu sana. Yesu aliwaponya vipofu wengine (Mt. 9:27-31; 20:29-34; Luka 18:35-43).

 

Haijulikani wazi ikiwa walikuwa vipofu kwa kuzaliwa, lakini Yohana 9:1 hufafanua bayana “mtu, kipofu tangu kuzaliwa.” Maelezo haya ni tofauti na visa vingine vya uponyaji wa vipofu. Jambo la kuvutia zaidi, Yesu alitumia mambo ya kawaida ya uchafu, mate, na maji. Haikuwa njia, bali Chanzo cha uhai, kilichomfanya mtu huyo aone.

 

Kwa maneno mengine, Yesu aliponya zaidi ya macho tu. Matibabu ya kisasa kama vile tiba kwa njia ya vinasaba yanaweza kuwaponya watu kimwili. Lakini kile kilichotokea katika birika la Siloamu kinaelekeza kwenye badiliko la ajabu la akili. Sio tu kwamba seli za macho ziliponywa na mifumo ya fahamu kuimarishwa, bali ubongo ulijazwa na uwezo, kumbukumbu, na uwezo wa kuchakata mtiririko mpya wa taarifa.

 

Wakati wanafunzi na Mafarisayo walikuwa wakikazia kujua sababu ya upofu, Yesu alitumia tukio hilo kufundisha lengo lake: wote wanahitaji mabadiliko makubwa na kamili ya kimwili, kiakili, na kiroho kutoka juu. Ulemavu huku ukikubali hitaji la Yesu ni bora zaidi kuliko kuwa timamu bila Yesu. Anasema, “Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, ‘Twaona.’ Basi dhambi yenu inakaa” (Yohana 9:41).

Alfred Kwasi Asiem, mkurugenzi wa vijana wa Divisheni ya Afrika Magharibi-Kati (WAD), akimbatiza Mtafutanjia wakati wa Kambi la 4 la Watafutanjia la WAD lililofanyika Desemba 24-30 katika Chuo Kikuu cha Valley View huko Oyibi, Accra, Ghana.

“Tuna furaha kuanza ukurasa huu mpya katika safari yetu ya utangazaji. Hebu tuendelee kuomba na kuunga mkono Hope Channel Central Philippines tunapojitoa kuzalisha programu zenye matokeo kupitia jukwaa hili la kidijitali.”

—Denison Grellmann, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) Australia, juu ya kazi ambayo timu yake imekuwa ikijihusisha nayo. Ingawa ADRA Australia ilianzishwa mwaka wa 1984, Kanisa la Waadventista lilikuwa tayari limepanga shughuli za misaada tangu 1918, wakati lilipotuma misaada maeneo yaliyoharibiwa na Vita vya Kwanza vya Dunia.

Idadi ya washiriki waliomaliza kozi ya uzinduzi ya Uamsho mwezi Novemba mwaka 2023. Uamsho ni programu ya Divisheni ya Pasifiki Kusini kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Avondale. Programu hii inafafanuliwa kama tukio la uanafunzi, kozi ya wiki 12, isiyotambulika rasmi ni kwa ajili ya wale ambao wana shauku ya kumtumikia Mungu na wana nia ya kujifunza na kupata elimu na ujuzi ili kufanya-wanafunzi.

Ulemavu ndani ya Kanisa la Waadventista

Washiriki wa kanisa waliulizwa ni aina gani ya ulemavu wowote walio nao.

“Tunapotafakari juu ya miaka 40 ya ADRA nchini Australia, tunashukuru kwa kila mwezeshaji, mtu wa kujitolea, mwajiriwa, mjumbe wa bodi, na bila shaka, Kanisa la Waadventista wa Sabato. . . . Sasa hivi tunafanya kazi katika nchi 25 . . ., tunaendelea pia kuongeza kasi ya mpango wetu wa kitaifa. Sasa hivi kuna zaidi ya miradi 100 nchini Australia, na hii inawezekanaa tu kwa msaada wa wafanyakazi wetu zaidi ya 2,000 wa kujitolea, na ushirikiano na makanisa na maduka ya ADRA [maduka ya kuhifadhi bidhaa] kote nchini.”

—Denison Grellmann, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) Australia, juu ya kazi ambayo timu yake imekuwa ikijihusisha nayo. Ingawa ADRA Australia ilianzishwa mwaka wa 1984, Kanisa la Waadventista lilikuwa tayari limepanga shughuli za misaada tangu 1918, wakati lilipotuma misaada maeneo yaliyoharibiwa na Vita vya Kwanza vya Dunia.

30

Idadi ya wahitimu waliomaliza programu ya kwanza ya LeadLab katika Divisheni ya Kusini mwa Asia-Pasifiki. Warsha ya Uongozi Ulimwenguni ya kanisa ilizindua mpango mkubwa wa uongozi na maendeleo ambao uliwaleta pamoja viongozi kutoka nyanja mbalimbali za huduma ndani ya mashirika na taasisi za Waadventista. LeadLab imekuwa nguzo ya kuandaa wazee, kuimarisha msingi wao wa maadili, na kuthibitisha tena makusudi yao ya huduma.

“Ushirikiano huu pamoja na AdventHealth ni ombi lililojibiwa. Hatuoni AdventHealth kama mshirika tu bali kama sehemu ya familia yetu.

—Alexis Pérez Zúñiga, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya del Sureste, juu ya ushirikiano mpya kati ya hospitali ya Meksiko na mtandao wa afya wa Marekani. Hospitali ya del Sureste ni taasisi ya huduma ya afya ya Waadventista iliyoko katika jiji la Villahermosa, Tabasco, Meksiko na huhudumia takribani wagonjwa 8,000 kila mwaka na timu ya zaidi ya wafanyakazi 200.

10

Idadi ya miaka ambayo kanisa la Vivo limekuwa likikua huko Geneva, Switzerland. Kanisa liliadhimisha siku ya yake ya ukumbusho wa miaka 10 siku ya Sabato, Januari 13. Kanisa lilianzishwa kama sehemu ya mpango wa “Tumaini kwa Miji Mikubwa” ambao ulizinduliwa mwaka 2005 katika Kikao cha 58 cha Konferensi Kuu huko St. Louis, Missouri, Marekani. Miaka minane baadaye, mwaka 2013, wanachama wa Geneva waliomba ufadhili wa fedha. Mradi huo uliidhinishwa, na Januari 11, 2014, huduma ya kwanza ya Vivo ilifanyika.

“Kuwafikia watu wa kidunia na wanaoukataa Ukristo ni mojawapo ya changamoto kubwa za utume wa Kanisa la Waadventista. Ni mojawapo ya maeneo matatu ya Kurejelea Utume tunayoyazingatia—pamoja na eneo la 10/40 na eneo la Mjini. Brendan Pratt analeta uzoefu mzuri wa kuwahudumia watu hawa nchini Australia na New Zealand, na najua ataleta njozi yenye nguvu na ya vitendo katika kituo cha Utume Ulimwenguni.”

– Gary Krause, mkurugenzi wa Utume wa Waadventista wa Ofisi ya Konferensi Kuu, kuhusu Brendan Pratt ambaye ni mkurugenzi mpya wa kituo cha Utume Ulimwenguni kwa ajili ya Utume kwa watu wa Kidunia na wanaoukataa Ukristo. Pratt ni mchungaji mwenye shauku ya kumshiriki Mungu pamoja na watu wa kidunia na kwa watu wanaoukataa Ukristo. Atasimamia juhudi zinazokua za Kanisa la Waadventista ili kufikia kundi moja la watu duniani kote.

Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Cuba linaongeza mara dufu juhudi zake za kuwaandaa vijana katika kukabiliana na kuondoka kwa idadi kubwa ya wachungaji na viongozi wa maeneo mahalia katika miaka ya hivi karibuni. Kabla ya ugonjwa tandavu wa UVIKO-19, kuhama kwa wachungaji na viongozi wa makanisa lilikuwa tukio la kawaida, lakini idadi hiyo imekua kwa kiwango kisicho cha kawaida tangu wakati huo, viongozi wa kanisa mahalia walisema.

 

“Kati ya mwaka 2021 na mwaka 2023 migogoro ya aina tofauti kisiwani ilichipuza kuhama, jambo ambalo limeathiri Kanisa la Waadventista hapa,” Aldo Pérez, mwenyekiti wa Unioni Konferensi ya Cuba, alisema. “Tumepoteza wachungaji wa thamani na viongozi mahalia.” Katika mwaka 2023 pekee, familia 29 za wachungaji ziliondoka kisiwani. Tangu 2021, familia 44 za wachungaji—moja kati ya familia tatu—zimeondoka kwenye kituo cha kazi.

 

 

MPANGO WA DHARURA WA MAFUNZO

Hali iliyokuwa ikiongezeka iliwalazimu viongozi kutekeleza kile wanachokiita mpango wa dharura wa kutoa mafunzo kwa viongozi wapya. “Tuna viongozi wachanga kanisani, na lazima tuwaandae vyema ili kanisa liweze kusonga mbele,” Pérez alisema.

 

Ili kukabiliana na changamoto ya kupungukiwa wachungaji na viongozi wengi mahalia, viongozi wamepanga mikakati ya kutoa mafunzo kwa vijana 7,000, wakiwemo Viongozi Wakuu wapya 3,500 na Viongozi Waadventista (AY) 3,500 kote kisiwani.

 

“Lengo ni kuchipuza michakato na kuzalisha viongozi waliofunzwa na waliohamasishwa ili kuhudumu kwa kasi kubwa na kwa wingi kushinda wimbi la kuhama,” Ray Frometa, mkurugenzi wa Idara ya Vijana Unioni ya Cuba, alisema.

 

Wakati wa mafunzo ya hivi karibuni ya viongozi wa vijana zaidi ya 500 na wanafunzi wa Huduma za Kampasi za Umma (PCM) na wanataaluma vijana mwezi Januari, Frometa aliwahimiza kujitahidi kuleta mabadiliko kwa ajili ya Bwana na kamwe wasifikirie wala kusema kwamba viongozi bora wameondoka nchini. “Sisi tuliobaki ndio ambao Mungu atawatumia kumaliza kazi,” alisema. “Kazi hii siyo juu ya kipawa cha mwanadamu, bali ni juu ya mapenzi na kusudi la Mungu.”

 

 

KUWAIMARISHA VIONGOZI WA VIJANA

Kama sehemu ya mkakati wa kurejesha uongozi, mchungaji ameteuliwa katika kila makongamano 20 ya AY kote nchini. Kila mmoja wao anaweza kusimamia moja kwa moja na kuongoza katika mchakato wa uandikishaji na mafunzo ya viongozi wapya wa AY na Viongozi Wakuu, Frometa alisema. “Watakuwa na kazi maalumu ya kusisitiza uanzishaji wa vyama na viongozi wa vijana pamoja na programu ya ushauri ambayo itaishia kuwajumuisha katika uongozi mahalia wa kanisa,” alieleza. “Kuwa sehemu ya timu ya uongozi iliyoratibiwa kitaifa, yeyote kati yao anaweza kuendelea kufanya kazi na mikakati iliyowekwa na hatimaye kuwa tayari kukabiliana na wimbi la kuhama katika konferensi au misheni yoyote nchini.”

 

 

VIONGOZI WALIOJITOA NA WENYE SHAUKU

Kuwanoa vijana katika viwango tofauti na huduma za kanisa inasalia kuwa kipaumbele na sehemu ya mkakati unaoendelea, Pérez alisisitiza. Mwezi Januari tarehe 12 na 13, karibu wanafunzi 400 wa vyuo vikuu, wataalamu vijana, na wanafunzi wa shule za sekondari walikusanyika Las Tunas kwa ajili ya tukio la PCM, ambapo walikumbushwa kuambatana na Mungu na kuwahudumia wengine hata kati ya changamoto wanazokabiliana nazo kila siku.

Hakuna uhaba wa miujiza nchini Cuba, Pérez alisema. “Mungu ataendelea kufanya miujiza zaidi hapa Cuba, hasa ili viongozi wetu vijana waliofunzwa waweze kuendelea kuleta vijana wengine kwa ajili ya ufalme wa milele.”

Uongozi mpya wa Konferensi ya Kusini mwa Uingereza (SEC) ulianza tarehe 9 Januari kwenye Maonyesho yao ya kila mwaka ya Uinjilisti, yaliyofanyika katika Chuo cha Elimu ya Juu cha Newbold huko Bracknell.

 

Katika muda wa miezi minne tu tangu kuingia madarakani, viongozi hao, pamoja na wakuu wa idara, wameshiriki katika mazungumzo ya kina, maombi, na mashauriano ili kupanga mwelekeo mpya wa konferensi. Mwelekeo wa safari yao usingeweza kueleweka. “Kristo katika mioyo yetu. Kristo katika nyumba zetu. Kristo katika makanisa yetu. Kristo mitaani.”

 

Itazame hii—siku yenye baridi kali Jumapili ya kwanza ya mwezi Januari huko Berkshire, huku washiriki wengi wakisafiri kwa saa mbili hadi nne toka eneo moja hadi eneo lingine ili kukusanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Newbold kufikia saa 04:00 Asubuhi. Takribani viongozi mahalia 1,000, wakisukumwa na kujitoa kwao kwa ajili ya utume, walikusanyika ili kuchunguza jinsi ya kujumuisha thamani hizi katikati ya ulimwengu unaobadilika kwa kasi unaowazunguka.

 

Kwa viongozi, Maonyesho ya Uinjilisti yalifafanua zaidi ya “jinsi ya” na mawazo mapya. Yalishughulika na badiliko na “mabadiliko ya dhana,” ikishughulikia ukweli mpya wa utamaduni unaozunguka kanisa.

 

“Ni muhimu sana kwetu kufahamu hili,” alisema Roger Hernandez, mkurugenzi wa huduma na uinjilisti wa Unioni Konferensi ya Kusini, Marekani, na mzungumzaji mkuu wa kwanza. Akimnukuu Dan White, mwanzilishi wa kanisa huko Marekani, Hernandez alisisitiza umuhimu wa kuelewa jinsi imani za Kikristo zinavyokingamana na utamaduni unaopingwa na “ukweli kamili,” “midahalo,” “upingaji” wa vikundi, “uhifadhi wa itikadi za mipaka,” na “kutia aibu” ili kutenganisha.

 

Mhudumu mwenza wa Hernandez na mke wake, Kathy, aliyebobea katika huduma ya ukarimu, alirejea njozi yao katika video waliyoshiriki wakati wa uwasilishaji, ikionyesha hitaji la kutoa huduma zaidi ya salamu rahisi kwa wageni.

Karen Glassford, meneja wa uinjilisti wa kidijitali wa Huduma za Mawasiliano na Vyombo vya Habari Konferensi Kuu (GC), alifanya vivyo hivyo. Alisisitiza ukuaji wa haraka wa uinjilisti wa kidijitali na kuanzisha mradi pamoja na idara ya mawasiliano na vyombo vya habari ya SEC ili kuendesha mifano ya uinjilisti wa kidijitali kwa makanisa yaliyochaguliwa. Matokeo yanayoweza kuonekana ya mradi huu katika kuunganishwa na jamii inayoongezeka mtandaoni yalisifiwa na waliohudhuria kama vile Elizabeth Taslmacsi, Brighton, Hove, na mjumbe wa mtaa wa Worthing. “Watu wanaoishi katika miji yetu mikubwa na majiji wametengwa kabisa. Hatuwafahamu majirani zetu; tunaogopa kuzungumza juu ya imani yetu. . . . [Mpango huu] utatengeneza fursa kwa ajili ya ushirikishwaji zaidi wa washiriki,” alisema.

 

Kikao cha mwisho cha asubuhi, kikiongozwa na mwenyekiti wa SEC Kirk Thomas, kiliwasilisha ujumbe dhahiri: “Ni wakati wa kujifunza na kusonga mbele.” Alitoa wito wa kufanywa upya, kukua, na utayari wa kukubali mabadiliko. Thomas aliwahimiza viongozi “Ondoka” na “Hamasishwa kwa ajili ya Utume,” akimsisitiza Kristo kama kitovu cha mkakati wa SEC.

 

Siku ilipokuwa ikiendelea, warsha 23, ambazo hasa ziliendeshwa na viongozi wa SEC na wakurugenzi wa idara, ziliwapa viongozi wa eneo mahalia nafasi ya kushirikiana na uongozi mpya.

Akizungumzia warsha yenye ufanisi ya uinjilisti wa kidijitali, Bernie Holford, aliyeteuliwa hivi karibuni kama mchungaji wa kanisa la Hemel Hempstead, alisema, “Kama mzee ambaye sijajishughulisha sana na Facebook, nimegundua jinsi mbinu ya uinjilisti wa kidijitali inavyoweza kuwa.”

 

Siku ilihitimishwa kwa washiriki kuchangamana na kuungana tena baada ya warsha, kutembelea duka la nyumba ya uchapishaji ya Stanborough, na kutazama maonyesho mbalimbali ya utume.

“Njozi inaendelea,” viongozi wa kanisa walisema. “Kristo katika mioyo yetu, nyumbani mwetu, kanisani kwetu, na kwenye mitaa. Ni njozi inayoanza na Kristo ndani ya mioyo yetu.”

Kituo cha ushuhudiaji katika kitongoji chenye majani mengi cha Melbourne, Victoria, Australia, kinawafikia wanafunzi wa chuo kikuu na majirani na kuwapatia zana za afya bora ya kimwili, kiakili, kiroho, kihisia, na kijamii.

 

Kituo cha Ustawi cha weExplore, mpango uliojikita katika ufadhili wa Gateway Adventist Centre, kituo cha jamii kisichokuwa cha kibiashara huko Melbourne, kimekuwa kikiwasaidia mamia ya wanafunzi wanaohudhuria karibu na Chuo Kikuu cha Monash na wengine katika jamii kupokea msaada wa chakula na kujiandikisha katika kozi za bure zinazoshughulikia mada za ustahimilivu wa akili na mwenendo unaofaa katika kuzuia ugonjwa wa kisukari.

 

“Kituo [hicho] cha weExplore kinahudumu kama mpango wa kupanda mbegu, kujenga ufahamu katika jamii kwa sababu tunataka kuifikia jamii,” mfanyakazi wa kujitolea Gordon Chau alieleza nje ya Mkutano wa Vijana Waadventista wa mwaka 2024 (AYC) huko Melbourne mwezi Januari. “Tunataka kuwategemeza watu, kuwasaidia, na bila shaka, hatimaye, kuwaleta kwa Kristo.”

 

Mpango huo, Chau anasema, unaanzia katika urafiki kwenda huduma za kanisani, kujifunza Biblia hadi kuongoa na kulea. “Baadhi ya wafanyakazi wetu wa kujitolea walipita katika kituo chetu na kusema, ‘Hiki ni nini?’ ” alisema. Chau alisimulia kisa cha Kavitha, mama wa mapacha wa kiume aliyetengwa ambaye wakati mmoja aliwahi kuvutiwa akasimama ili kutaka kujua.  Kavitha alihisi kutendewa kwa ukarimu na baadaye akaomba Biblia. Muda fulani baadaye alijiandikisha katika masomo ya kujifunza Biblia, hatimaye akabatizwa, na sasa anajitolea ili kutoa mafunzo kwa wengine. “Ni aina ya mduara,” Chau alieleza. “Wale waliohudumiwa sasa wanawahudumia wengine.”

 

 

KITUO CHA USHUHUDIAJI MJINI

Wazo la kufungua Kituo cha Ustawi cha weExplore lilianzishwa Aprili 2018 kwa sababu ya kikao cha maombi na mipango cha Gateway Adventist Centre. “Hapo awali tulikuwa na fedha za Utume Ulimwenguni, na zilitusaidia kuanzisha kituo,” Leanne Tilson, makamu mwenyekiti wa chama na mratibu wa programu za huduma hiyo, alisema. “Tulikuwa tukiomba juu ya hilo kama kanisa, mara tulipokuwa na njozi ya kuanzisha kituo cha ushawishi ndani ya miaka mitatu. Lakini chini ya miezi sita Bwana alileta fedha hizi. Alitufungulia mlango, hata tulipokuwa hatujajiandaa na tulipokuwa tukifikiria kwa muda mrefu zaidi,” Tilson alisema.

 

Kwa mujibu wa tovuti ya kituo hicho, “tangu kuanzishwa kwa weExplore, kalenda yetu imejawa na matukio ya kusisimua kama yalivyoungwa mkono na misaada na michango. Madaktari na wataalamu wengine wa afya hujitolea wakati wao wa thamani. . . . Tunaona wengi katika jamii yetu pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu wakishuka kituoni na . . . kueleza mahitaji yao ya afya bora na kamili kabisa.”

 

Tovuti hiyo pia inaeleza kwamba kwa sababu ya athari za UVIKO-19, “afya ya akili na ustawi wa hisia ndiyo mada kuu kwa wakati huu.” Inaongeza, “Tumekuwa tukitumia jukwaa la mtandaoni kutoa msaada na uangalizi kwa jamii yetu, pamoja na huduma binafsi.”

 

Kituo hicho kipo kimkakati katika umbali wa kutembea wa Chuo Kikuu cha Monash, ambacho kina idadi ya wanafunzi zaidi ya 85,000. Shukrani kwa makubaliano na serikali ya Victoria, kituo hicho kinatoa mifuko ya chakula kwa takribani wanafunzi 300 kwa juma. Kituo hiki kinaandikisha watu wa kujitolea wapatao 75 kutoka katika Konferensi nne za Waadventista huko Melbourne na katika jamii. Programu za afya ya mwili na akili, ikijumuisha darasa la kila juma la mazoezi ya mwili, ni maarufu sana.

Na vipi kuhusu Kavitha, mwanamke ambaye alisimamishwa na kituo na hatimaye akawa mshiriki wa kanisa la Waadventista na mfanyakazi wa kujitolea wa kituo hicho? “Natamani ningesikiliza mapema,” Hivi karibuni Kavitha alisema. “Kumpata Yesu na kutoa maisha yangu kwake kumeleta badiliko kamili.”

Katikati ya Sarawak, Malaysia, huduma ya ufundi wa kuchezesha karagosi ya Chai Sew Moi imekuwa ikiamsha uhamasishaji kwa watu wanaomzunguka kwa miaka mingi. Amekuwa na mguso sana kwa wengine kisanii na kiroho tangu alipostaafu mwaka 2016 na ametumia vipawa vyake kushiriki imani ya Mungu na watoto kanisani na katika jamii mahalia.

 

Safari ya Moi katika ufundi wa kuchezesha karagosi ilianza kwa wastani. Mwaka 1993, alifanya uamuzi wa kujaribu bahati yake katika ufundi wa kuchezesha karagosi baada ya kutazama kipindi cha Kimarekani cha Sesame Street pamoja na mpwa wake wa kike katika miaka ya 1970 na baadaye na watoto wake mwenyewe. Bila mafunzo rasmi, aliumba wahusika wa karagosi kwa ajili ya programu ya Shule ya Sabato, lengo likiwa ni kutangaza sadaka za utume wa kanisa. Huduma yake mpya ilianza kupata kasi alipowashirikisha watoto wenye umri wa miaka tisa kama wachezesha karagosi na waigiza sauti.

 

Tangu siku hizo za mwanzo, huduma ya ufundi wa kuchezesha karagosi katika kanisa lake imekua kwa kasi. Watoto wakawa washiriki hai wa shughuli za uongozi wa nyimbo, shughuli za kanisa na programu maalum, zote zikionyesha ufundi wa kuchezesha karagosi. Moja ya mchezo wa karagosi unaojulikana sana wa Moi ni, “Hobart the Worm: Tumeumbwa kwa Uzuri,” ulioleta ujumbe kwamba kila kitu kilichoumbwa na Mungu ni muhimu. Uonyeshaji huu ulivuka mipaka ya nchi, na maonyesho yake yalifikia nchi zikiwemo Ufilipino, Indonesia, Myanmar, Korea, Taiwani na Mongolia.

 

Kama mwalimu wa shule wa zamani, Moi aliongeza shauku yake kwa wenzake, kuwafundisha jinsi ya kutumia karagosi kama zana ya kufundishia yenye ufanisi. Mwaka 1998, alipokea mafunzo rasmi ya ufundi wa kuchezesha karagosi katika mkutano wa Huduma za Watoto na baadaye alijifunza kutoka kwa wachezesha karagosi wataalamu kutoka Marekani na Australia.

 

Mwaka 2021, katikati ya changamoto za ugonjwa tandavu wa UVIKO-19, Moi alipata njia ya kipekee ya kuleta furaha na tumaini. Alianzisha mbio za masafa marefu za siku 100 za uimbaji wa karagosi, akishiriki nyimbo za kidini zilizoombwa na marafiki na familia. Mpango huu ulihudumu kama kioleza cha tumaini wakati wa kipindi chenye changamoto.

 

Kwa wakati huo huo, Moi alitambulisha jukwaa la video za karagosi lenye dhamira, ikiwa ni pamoja na, “Bustani ya Sifa,” “Kituo cha Injili,” na “Baraka za Mwisho wa Mwaka,” zote zikiwa na lengo la kusambaza furaha, tumaini, na upendo wakati wa changamoto za mwaka 2021.

 

Matokeo ya Moi kwa watoto hayapimiki. “Watoto wamepokea ufundi wa kuchezesha karagosi mara moja, bila kusita. Kuwasilisha maonyesho ya karagosi ni njia ya kuaminika ya kuvuta usikivu wa mtoto,” alisema. Wakati baadhi mwanzoni walikuwa na mashaka kuhusu karagosi, punde waligundua uwezo wake wa kufikisha kweli za Kibiblia na mafundisho ya maadili.

 

Alikuwa mwasisi katika mataifa kadhaa ya Kusini Mashariki mwa Asia, shukrani kwa imani yake iliyojikita katika utume wa Mungu. Moi aliwasilisha ufundi wa kuchezesha karagosi na kutengeneza karagosi katika warsha wakati wa mikutano na semina ili kushiriki zawadi hii na wengine wanaotaka kuwafikia watoto. Uthabiti na juhudi zake hatimaye zilileta matokeo ya kuumba na kusambaza makaragosi ishirini na nne katika mashirika nane ya Waadventista ya Kusini Mashariki mwa Asia.

 

Kutumia makaragosi kanisani, Moi anaamini, kunaweza kusaidia watoto na watu wazima kuunganisha imani yao kwa kiwango kikubwa. Hakika, huduma ya ufundi wa kuchezesha karagosi inakua kwa kasi kanisani, ikitoa aina ya burudani ya kisasa wakati wa kufikisha ujumbe wa thamani wa kiroho.

 

“Watoto ni zawadi kutoka kwa Bwana,” Moi anasema, akimnukuu mtaalamu wa elimu ya Kikristo, David Faust. “Hebu tushughulikie zawadi hii kwa uangalifu. Hebu tujali sana kuhusu watoto ili tuwahudumie kulingana na mahitaji yao. Hebu tuwafundishe kweli za Kibiblia. Hebu tuwaongoze wapate kufurahia kwa njia nzuri na safi. Hebu tutumie karagosi na maonyesho kuleta ubora kama wa watoto ndani yetu sote.”

Katika majira ya joto ya mwaka 1992, mke wangu alikuwa mkurugenzi wa kituo cha Early Childhood katika Shule yetu ya Waadventista huko Wenatchee, Washington. Nilikuwa nimehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Walla Walla na shahada yangu katika teolojia na nilialikwa kuhudumu kama mchungaji wa vijana kwa majira hayo ya joto katika Kanisa la Waadventista wa Sabato la Wenatchee. Mwaliko ulikuja na sharti moja—ilinipasa kujifunza kuendesha basi la shule na kupita mitihani ya kuandika na ya uendeshaji ili nipate leseni yangu ya kuendesha gari la kibiashara. Kwa hiyo, punde nilikuwa na uzoefu kama wa Yona kumezwa na “nyangumi mkubwa” mwenye rangi ya njano—basi la shule.

 

Kwa ninavyokumbuka, hili lilikuwa basi aina ya C-180 la mwaka 1965 lililotengenezwa na Gillig Brothers na lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 52. Lilikuwa na breki za upepo na muundo wa gia ya mkono ya namba RT610 10 ambalo si otomatiki. Na lilikuwa na klachi ya mara mbili. Hicho ni nini? Naam, unapoendesha gari lenye mkondo wa mafuta wa mkono, mguu wako wa kushoto hutumika kukanyaga klachi ili kubadilisha gia. Ikiwa gari lina klachi ya mara mbili, lazima ubonyeze klachi mara mbili ili kubadilisha gia. Kwa nini mara mbili? Mara ya kwanza kwa kubadilisha kutoka gia iliyopo na mara ya pili, kuingiza gia inayofuata. Kujifunza kuendesha basi katikati ya mjini na kufika kwenye taa za kusimamisha lilikuwa zoezi la viungo. Ilionekana kutokuwa rahisi kwangu, lakini kwa majira hayo ya joto, niliendeleza mazoezi ya kukanyaga mara mbili! Na nilifaulu mtihani wangu wa kuendesha!

WITO WA KUJALI NA KUWASHIRIKISHA

Kristo aliwaita wanafunzi Wake kujifunza “kukanyaga mara mbili” kwa kuona uwezekano wa watu wote, pamoja na watu wenye ulemavu na wale waliotengwa.

 

Wanafunzi walikuwa na mawazo yasiyo sahihi kuhusu jinsi huduma ya Yesu ilivyopaswa kuwa. Matarajio haya yalikinzana na wito wa Kristo wa kuwajali wengine na kuwashirikisha katika kazi ya Mungu. Wanafunzi walilazimika kujifunza  “kukanyaga mara mbili” ili kuendeleza imani yao. Hatua ya kwanza ilikuwa kutoa mawazo yao kuhusu ufalme wa Mungu ulivyotegemewa na kuelewa vipaumbele halisi vya ufalme wa Mungu. Hii haikuwa ya asili kwa Petro, Yakobo au Yohana. Wakati Yesu akiwa wazi kuhusu utume wake na jinsi ulivyohusisha watu wenye uwezekano, wanafunzi walitatanika, kama inavyoonekana katika Yohana 9:1-3.

 

“Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.”

Yesu alionyesha mfano, kwa wanafunzi Wake, njia tofauti ya kuwatazama watu. Badala ya kuzingatia ulemavu wa mtu huyu, Kristo aliona uwezekano wa jinsi mtu huyu anavyoweza kuwa shahidi wa neema ya Mungu inayotenda kazi. Yesu alikabiliana na teolojia potofu ya wanafunzi kuhusu ulemavu na kuwasaidia kuona uwezekano. Aliwasaidia wanafunzi Wake kuendeleza matendohiari ya imani yao na kujiondoa kutoka katika shutuma hii.

 

 

JARIBIO LA TABIA

Katika Mathayo 25:31-46, tunaona wazi wito wa Kristo wa kuhudumu kwa “hao walio wadogo.”

 

Ellen White anaongezea zaidi jaribio hili kwa kujali na kuhusisha anapoandika:

“Nikaona kwamba ni majaliwa ya Mungu kwamba wajane na yatima, vipofu, viziwi, vilema na watu wanaotaabika kwa njia mbalimbali, wamewekwa katika uhusiano wa karibu wa Kikristo na kanisa Lake; ni kwa ajili ya kuwathibitisha watu Wake na kukuza tabia yao ya kweli. Malaika wa Mungu wanatazama kuona jinsi tunavyowatendea watu hawa wanaohitaji huruma yetu, upendo na ukarimu. Hili ndilo jaribio la Mungu kwa tabia zetu. Ikiwa tunayo dini ya kweli ya Biblia, tutahisi kwamba deni la upendo, wema na maslahi linastahili kwa Kristo kwa niaba ya ndugu Zake; na hatuwezi kufanya lililo dogo kuliko kuonyesha shukrani zetu kwa upendo Wake usio na kipimo kwetu tulipokuwa wenye dhambi tusiostahili neema Yake, kwa kuwa na moyo wa kupenda na upendo usio na ubinafsi kwa wale ambao ni ndugu zetu na ambao wana bahati mbaya kuliko sisi.”1

“Mungu ataliwajibisha kanisa—kama mwili, kwa ajili ya mwenendo mbaya wa washiriki wake. Ikiwa roho ya ubinafsi na isiyohurumia imeruhusiwa kuwepo kwa mshiriki wake yeyote kwa wanaohitaji huruma, mjane, yatima, kipofu, kilema au wale ambao ni wagonjwa wa mwili au akili, ataficha uso Wake kutoka kwa watu Wake mpaka watakapotekeleza wajibu wao na kuondoa ubaya uliopo miongoni mwao. Ikiwa yeyote anayelikiri jina la Kristo na kumwasilisha visivyo Mwokozi wao kiasi cha kutojali wajibu wao kwa wanaoteseka, au ikiwa kwa njia yoyote wanajaribu kujinufaisha wenyewe kwa kudhuru wenye shida na hivyo kuwaibia njia za kujipatia mali, Bwana atahesabu kanisa kuwa na dhambi ya washiriki wake mpaka watakapofanya yote wanayoweza kurekebisha uovu uliopo. Hatasikiliza sala ya watu Wake wakati yatima, aliyefiwa na baba, kilema, kipofu, na wagonjwa wanapuuzwa kati yao.”2

 

Baada ya kuondoa gia ya hofu na unyanyapaa, tunapaswa kuingiza gia ya upendo na kujumuisha. Tunapogundua uwezekano wa kumheshimu na kumtukuza Mungu ulio ndani ya wale wanaotengwa mara nyingi, tunakuwa kama Mungu tunayedai kumtumikia.

 

Hivyo, Yesu anatuita leo kujali na kuwahusisha wote. Mpango wa Huduma Wezeshi za Waadventista (APM) unatafuta kushiriki Ujumbe wa Malaika Watatu kwa na pamoja na vikundi vya watu saba ambavyo ni pamoja na:

  1. Jamii ya viziwi na watu ambao wamepoteza uwezo wa kusikia.
  2. Watu ambao ni vipofu au wasioona vizuri.
  3. Watoto yatima na wale walio hatarini ambao ni pamoja na watoto wa mitaani, watoto wa kulelewa, watoto wahamiaji na wakimbizi, na watoto ambao mzazi wao yupo gerezani.
  4. Watu wenye changamoto za afya na ustawi wa mwili.
  5. Watu wenye changamoto za afya na ustawi wa akili. Hii ni pamoja na matatizo ya akili na changamoto za maendeleo ya akili kama vile ugonjwa wa akili kwa watoto na kromosomu za ziada.
  6. Watu wenye uzoefu wa kupoteza wenzi wao (wajane wanawake, wajane wanaume, na wenye uzoefu wa kupewa talaka, kuachwa, n.k.).
  7. Wanaotoa huduma kwa makundi haya.

Kupitia Huduma Wezeshi za Waadventista, makanisa mahalia pamoja na vikundi saba tofauti vya watu vinaweza kuhudumu kwa ajili ya matokeo makubwa zaidi ya utume. Kaulimbiu yetu ni “Wote wana vipaji, wanahitajika na wanathaminiwa.”

 

 

KWA HIVYO? NINI SASA?

Mawazo na maswali machache ya kutumia kwa ajili ya tafakari yako. Kote ulimwenguni, serikali na jamii zimepuuza, zimetenga, au kunyanyapaa jamii ya viziwi, watu wenye ulemavu na wale walioteseka kwa kupoteza mwenzi. Ninaamini kwamba, Kanisa la Waadventista wa Sabato lina jukumu la kufanya hapa katika nyakati za mwisho kwa kuleta ufahamu, kukubalika na matokeo—mkakati wa “A Tatu” (awareness-Kutambua, acceptance-Kukubali, na action-Kutenda) wa Huduma Wezeshi.3

 

Basi, tutaitikiaje mwito wa Roho wa Mungu? Je, tutaweza kuendeleza matendohiari ya imani yetu ili kuona uwezekano ambapo wengine huona ulemavu, udhaifu na ukomo? Tutafaulu huo “mtihani wa mwisho” katika Siku ya Hukumu? Ujumbe wa Malaika Watatu utatuhamasishaje kutunza wengine na kufanya kazi pamoja nao kwa njia za vitendo?

 

Katika familia yako ya imani ya kanisa lako mahalia, kanisa lako linahusishaje watu wenye uwezekano? Kanisa lako limesheheni vipi ubunifu wao, imani na uhai, na vipaji vya kiroho walivyopewa na Mungu?

 

Itakuwaje wewe na mimi kuendeleza matendohiari ya imani na kujifunza kukanyaga mara mbili? Ninataka kufanya sehemu yangu! Wewe je? Hebu tuendelee kueneza mwito wa siku za mwisho wa Kristo na kuwajumuisha watu wenye uwezekano tunawapohubiri injili ya milele “hao wakaao juu ya nchi—na kila taifa na kabila na lugha na jamaa” (Ufu. 14:6, msisistizo umeongezwa).

Akizaliwa New York, Marekani, Oktoba 11, 1871, DeGrove Turk alimwoa Grace A. Shear (aliyezaliwa Novemba 3, 1876) mnamo Desemba 28, 1903, huko Binghamton, New York. Walijiunga na Kanisa la Waadventista wa Sabato mnamo 19071 na mwaka uo huo waliripoti kazi yao ya uinjilisti wa vitabu.2 Kufikia 1908 tunapata rekodi ya akina Turk wakijiunga na kazi ya uinjilisti kama waimbaji kwenye mkutano wa kambi huko Oneida, New York.3 Mwaka uliofuata, 1909, Grace alipokea leseni yake ya umishonari, na D. G. Turk aliwekewa mikono ya katika huduma ya injili.4 Waliendelea kusafiri pamoja wakiimba na kulihubiri Neno katika jimbo lote la New York.5

 

Alifariki akiwa na umri wa miaka 79 mnamo Mei 15, 1951, na mkewe alifariki miaka 15 baadaye, akiwa na umri wa miaka 90, mnamo Novemba 16, 1966. Sehemu ya tanzia yake inasema, “Ingawa Mzee Turk alikuwa kipofu kabla ya ndoa yake, yeye na mkewe walikuwa wakiimba sana na walitumia vipaji vyao katika kazi ya Bwana. Walisaidia katika kazi kadhaa za ibada na uinjilisti ambapo Kaka Turk alithibitisha kuwa mnenaji hodari na aliyeshawishi.

 

Mwenzi wake mwaminifu alihudumu kama macho kwake katika maandalizi ya mahubiri yake. . . . Isipokuwa wakati ambapo alichukua muda kwa ajili ya kazi za uinjilisti katika miji kadha ya New York, alihudumu kama mchungaji wa kanisa la Binghamton kwa miaka 25.”6

 

Huduma ya akina Turk ni ishara ya jinsi wote wamechaguliwa kwa ajili ya utume, na wote wamepewa karama, wanahitajika, na wanathaminiwa.

Mara tu baada ya kuhitimu mwaka wa 2005, mke wangu, rafiki yetu, na mimi tuliamua kujaribu kushiriki katika shindano la kuendesha baiskeli lililokuwa likifanyika karibu na tulipoishi Chattanooga, Tennessee, Marekani. Ilikuwa inaitwa "Three State Three Mountain Challenge" kwa sababu moja ya njia ilikuwa safari ya maili 100 kutoka Tennessee hadi Alabama, kisha kwenda Georgia, kurudi Tennessee, na kupanda vilima vitatu. Nilipokuwa nikishuka kwenye moja ya vilima hivyo, wakati nikizunguka kona na . . . Duuu. Nilielezwa kuwa niligonga gari lililokuwa likipanda kilima. Siwezi kukumbuka hili wala chochote kingine kuhusu ajali hiyo. Wapanda baiskeli watatu waliokuwa baada yangu wote walikuwa wataalamu wa tiba, na walijua mara moja jinsi ya kunisaidia kubaki hai. Kama matokeo ya ajali hiyo, hata hivyo, nilipooza kutoka kiunoni hadi chini, kunifanya niwe nimepooza maisha yangu yote. Nimekuwa nikitumia kiti cha magurudumu tangu wakati huo. Kutumia kiti cha magurudumu kwa ajili ya kusafiri kuna changamoto zake, lakini pia fursa zake.

 

 

UWEZESHWAJI NCHINI ZAMBIA

Nimepata fadhila kubwa sana kuwa mwanachama wa Huduma Wezeshi za Kiadventista(APM) Kikosi Kazi cha Afya na Ustawi wa kimwili/Ujongefu. APM ni mpango wa Kanisa la Waadventista wa Sabato wa kuwahudumia watu ambao mara zingine wanakuwa hawajumuishwi. Imekua na kuwa huduma ya sehemu saba inayojikita katika wale ambao wamepoteza wenzi wao, wale ambao ni vipofu au wenye macho dhaifu, wale wanaowatunza wengine, viziwi na wenye uwezo mdogo wa kusikia, mayatima na watoto walio katika mazingira hatarishi, wale wenye changamoto za afya ya kimwili/ujongefu, na wale wenye changamoto za afya ya akili. Licha ya changamoto zetu, APM inatangaza ukamilifu katika changamoto zetu.

 

Nilipokuwa mdogo, nilitumia miezi kadhaa Afrika, na kwa miaka mingi nimejaribu kurudi huko ili kushiriki sehemu hii ya uzoefu wangu wa utotoni na mke wangu. Unaweza kupiga picha ya msisimko wangu alipopata nafasi ya kuhudhuria mkutano katika Chuo Kikuu cha Waadventista cha Afrika huko Kenya! Muda mfupi baada ya kupokea mwaliko wake, tulipata fursa ya kuwasiliana na mkurugenzi wa APM wa Konferensi Kuu na kuwa mabalozi wa APM wakati wa safari yetu. Nilipokuwa nikipanga mipango mikubwa ya kusafiri kote Afrika na kumwonyesha mke wangu maeneo niliyokuwa nikiishi, Mungu, kwa hekima yake isiyo na kikomo, alibadilisha safari yetu na kutupangia muda zaidi Zambia.

 

Huko Zambia, wenyeji wetu wapendwa Vera na Coster walipanga ziara ya ukarimu kwenye ofisi ya Southern Zambia Union Conference huko Lusaka. Katika ofisi za Union, tulikutana bila kutarajia na mkurugenzi wa APM wa Union kabla hatujapangwa kuanza shughuli zetu za mabalozi wa APM (ingawa hakuna kitu katika mipango ya Mungu ambacho ni cha nasibu). Siku hiyo hiyo, mkurugenzi wa APM alijifunza jinsi ninavyotumia ubao wangu wa kupandia na kushuka kutoka nje na ndani ya gari, na kwa shauku alituendesha kukutana na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linalotetea mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa nchi nzima ya Zambia. Hawa wawili walikuwa wakifanya kazi pamoja kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu.

 

Kwa kuwa ziara ya siku hiyo ilitarajiwa kuwa fupi, mkurugenzi wa Union alitaka tuwepo ili kutoa mafunzo kwa mamia ya viongozi na wanachama wa APM katika Union ya Kusini mwa Zambia kabla ya kuondoka nchini. Uelewa wa kusisimua ulianza kunivutia kwamba Waadventista katika Union hii na katika nchi ya Zambia walikuwa na miradi mingi ya kusaidia wale wenye uhitaji!

 

Siku ya mafunzo ilipofika, tulishiriki wasilisho la kivitendo lililoendana na yale yaliyopo kwenye eneo hilo, na utangulizi wa zana za APM mtandaoni. Nakumbuka nilivyofurahishwa na jinsi kanisa lilivyokuwa rahisi kufikika mahali  tulipokusanyika. Niliona jinsi wanachama na viongozi walivyokuwa wakifanya mabadiliko kwa kusudi kwa ajili yangu na washiriki wengine wenye viti vya magurudumu, wale ambao walikuwa viziwi au wenye uwezo mdogo wa kusikia, na wale ambao walikuwa vipofu. Uwepo wa fursa tofauti tofauti katika nafasi ile ulikuwa wa kustaajabisha! Kila mtu alikuwa na hamu ya kusaidia, na ingawa nilikuwa naweza kufika mahali popote bila kuhitaji msaada wa wengine, nao walipenda kunisaidia hata hivyo.

 

Moja ya uzoefu wa kusisimua zaidi ambao uligusa moyo wangu sana ulitokea wakati kwaya ya watoto, wote wakivalia sare zenye nembo ya APM na nembo ya Huduma ya Waadventista Wasiosikia kwenye mashati na mavazi yao, waliposimama kuimba. Wakati muziki ulichezwa, walianza kutafsiri nyimbo kwa ishara kwetu, na mkufunzi wao kwa fahari aliwaongoza. Ilikuwa wazi kwamba malaika wa Mungu walikuwa hapo pamoja nao, wakiimba na kuonyesha ishara kwa pamoja. Kama ungekuwepo, nina hakika ungekuwa unapata ganzi la ngozi, kikonyezi kooni, na machozi machoni mwako, kama ilivyotokea kwetu.

MFANO WA MAKANISA MAWILI

Zamani za kale kulikuwa na makanisa mawili. Makanisa yote mawili yalikutana na na kumjua mtu aliyetumia kiti cha magurudumu. Kanisa moja lilikuwa kubwa sana na lilikuwa na jengo zuri, lakini lilikuwa na lifti ya zamani ambayo ilikuwa haiaminiki na ilikuwa ikiharibika mara kwa mara. Pia lilikuwa na viti vya mbao ambavyo havikuwaruhusu watumiaji wa viti vya magurudumu kukaa vizuri karibu na familia au marafiki zao. Kanisa lingine lilikuwa dogo na lilikuwa linakodi jengo kwa ibada zake. Hatimaye, washiriki wa kanisa dogo walinunua ardhi na kuanza kujenga jengo lao wenyewe.

 

Washiriki wa kanisa kubwa walipopata habari kuhusu matatizo ambayo lifti na viti vya kanisa vilikuwa vikimfanyia mtu aliye kwenye kiti cha magurudumu, walianza ukarabati, bila kuwauliza watumiaji wa viti vya magurudumu wanachohitaji. Kama sehemu ya ukarabati wao, hatimaye waliweka lifti mpya na kufanya ukarabati kwenye viti ili kuweka nafasi za lazima kwa watu wanaotumia viti vya magurudumu kukaa.

 

Kanisa dogo lilishauriana na mtumiaji wa kiti cha magurudumu na kujenga kanisa lenye ghorofa moja ambalo halikuwa na haja ya lifti. Walichagua viti vizuri na vinavyoweza kuhamishika badala ya viti vya kanisa. Kwa njia hii, mtu aliye kwenye kiti cha magurudumu angekuwa na uhuru wa kukaa mahali popote alipochagua na na yeyote katika kanisa. Kanisa dogo hata kilijenga ngazi kwenye eneo la mhubiri ili kuwapa watu wanaotumia viti vya magurudumu na wengine wenye changamoto za ujongefu kufika mimbarini.

 

Mafundisho kutoka kwa mifano hii ni mengi. Kuongeza tu lifti kwenye jengo la kanisa, kwa mfano, hakuleti uhakika wa kufikika au kuleta hali kuwa sehemu ya jamii ya kanisa. APM inakwenda zaidi ya ukarabati wa majengo ya kawaida. Ipo ili kuleta hali ya kuwa sehemu ya jamii kwa kutusaidia sisi sote kutambua kuwa kila mtu ana kipawa, anahitajika, na kuthaminika—kama nilivyokuta hali ya mambo kule Zambia. Ikiwa unataka kujua jinsi unavyoweza kuunda hisia ya kuwa sehemu ya jamii katika kanisa lako ambayo ni zaidi ya miundombinu tu, tovuti ya APM ina hojaji linalopatikana bure ambalo wanachama na viongozi wa kanisa wanaweza kutumia ikiwa watachagua kuwa na ufikikaji zaidi.*

 

Sote tunafahamu aya ya Biblia inayosema, "Hapo ndipo ule mwisho utakapokuja" (Mathayo 24:14). Lakini umewahi kusoma aya huku ukiizingatia  Warumi 10:14 na 15? Kwa kuwa Yesu atarudi wakati injili itakapowafikia watu wote ulimwenguni, bado kuna ulimwengu wa kufikiwa. Tunawapuuza akina nani ambao wanahitaji kusikia injili? Mara nyingi tunawaza kuhusu walio katika maeneo ya misitu ya mbali katika nchi zisizojulikana. Ingawa hii inaweza kuwa kweli, je, inawazekana tunampuuza mtu aliye karibu nasi ambaye ni kiziwi, na pia labda ni Mwadventista, lakini anahudhuria kanisa la Jumapili la eneo lao kwa sababu kuna wafasiri huko? Au muumini ambaye kamwe haji kanisani kwa sababu kuna ngazi nyingi na hataki kumsumbua yeyote? "Watamwaminije yeye ambaye hawajasikia habari zake" katika lugha yao ya alama, au braille?

Mungu hatabiriki. Wakati mwingine, Huchukua tukio la kusikitisha katika maisha ya mtu na kulitumia kuleta furaha kwa wengine wengi.

 

Miaka kadhaa iliyopita, nilihudumu kama mhazini wa Konferensi huko Bucharest, Romania. Siku moja, nilipofika ofisini, lango zito la mahali pa kuingilia lilitoka kwenye bawaba zake na kuniangukia. Mshtuko wa maumivu ulipopungua, akili yangu ilianza kwenda mbio: vipi kama ningelazimika kuishi kwenye kiti cha magurudumu maisha yangu yote. Ingawa sikuishia kwenye kiti cha magurudumu, Mungu alikuwa na mpango tofauti. Kupitia ajali hiyo, Alikuwa akiniandaa kwa ajili ya mradi mkubwa ambao, kama unga wa mkate unavyoumuka, ilikuwa miaka mitano ya kutengenezwa.

 

Baada ya kumaliza muda wangu kama mkurugenzi wa Shule ya Sabato na Huduma Binafsi katika Unioni ya Romania, nilihudumu kama mchungaji katika Kanisa la Grant huko Bucharest na kusubiri njozi kwa ajili ya utume kwa shauku na kusudi kubwa. Katika maombi, nilirudisha kumbukumbu za lango la konferensi. Hapo ilianza safari ya umishonari ambayo ingeshinda fikra zangu kubwa.

 

 

MENGI YATAKUJA

Pamoja na kijana mmoja katika kiti cha magurudumu, Aurel Burcea, ambaye alikuwa akiratibu gazeti la watu wenye ulemavu kwa miaka mingi, tuliazimia kutengeneza familia kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kimwili huko Bucharest. Tulimwomba Mungu alete watu 25 ili kuanzisha mradi huu. Miezi tisa baadaye, watu 11 tu waliokuwa na changamoto za kimwili walikuwa wamejiandikisha. Aurel alisisitiza kuanzisha mradi huo. “Lakini hatuna watu 25 walioandikishwa!” Nilipinga.

 

“Tukianza, mengi zaidi yatakuja!” alijibu kwa kujiamini. Nikiwa bado ninasumbuliwa na kutoweza kufikia lengo la watu 25, nilikubali lakini niliendelea kumsumbua Mungu kuhusu lengo letu. Katika tarehe ya mkutano wetu wa kwanza, Aprili 18, 2010, tuliingia kwenye bwalo lililokodiwa huko Bucharest na kuhesabu watu wenye ulemavu: kulikuwa na watu 25, pasipo kujumuisha watu waliowasaidia na watu waliojitolea. Mungu alikuwa amejibu!

 

Mazingira ya mikutano yalikuwa ya furaha tele na shauku kubwa. Mario Brito, Mwenyekiti wa Divisheni ya Ulaya Kati, alitutembelea na kututia moyo kupanua zaidi. Watu wenye ulemavu kutoka miji mikubwa na midogo kote nchini Romania walikuja kuona kile ambacho Inuka na Tembea, kilichoratibiwa awali chini ya ADRA Romania, kilihusu hasa. Walituomba tuanzishe matawi katika miji yao. Leo hii, tuna matawi 32 nchini kote, ambayo yanajumuisha karibu watu 4,000 wenye changamoto za kimwili. Na bado tunaendelea kupanuka. Idadi ya watu wanaojitolea, wengi wao kutoka katika Kanisa la Waadventista, ni zaidi ya 6,000. Mwaka 2024, tunapanga kuanzisha matawi mapya 8-10.

 

Nchini Romania tumesajiliwa kama watoa huduma chini ya Wizara ya Kazi, lakini kanisa husimamia taratibu zote. Kila tawi linaongozwa na mchungaji na mshiriki wa kawaida wa kanisa anayeunda kiini cha tawi. Wanawajibika kuratibu programu tulizo nazo pamoja na walezi wetu wakifungua kila kikao cha tawi kwa masomo ya kiroho yaliyojikita kwenye Maandiko. Miaka mitatu baada ya kuanzishwa kwa shirika la Inuka na Tembea, ushirika wa watu wenye ulemavu ulianzishwa, ambao sasa una zaidi ya watu 50 wenye shauku ya kiroho, ambao wengi wao si Waadventista wa Sabato.

 

Tumeanzisha Kituo cha Kutembea Huru kwa watu wenye ulemavu, cha kwanza cha aina yake nchini Romania. Kwa kufuatana na mchango wa vifaa vya walemavu ili kuwasafirisha hadi mahali ambapo hawakuweza kufika kwa usafiri wa umma usio rafiki, tumewasafirisha maelfu ya watu wenye changamoto za kimwili. Wengi wa wasafiri wetu wamekuwa wanachama wa Inuka na Tembea. Tunafurahia uhusiano mzuri na miji katika maeneo ambayo tuna huduma ya “teksi bila malipo.”

KURATIBU KWA AJILI YA KUFANYA

Kila mwaka, tunatoa siku saba za furaha, urafiki, na elimu katika makambi ya kila mwaka, ambapo karibu watu mia mbili kutoka kote nchini wanakuja kwa ajili ya matembezi, programu za kila siku za nyimbo, mashairi, visa vya maisha, semina mbalimbali, na shughuli za michezo. Mwishoni mwa kambi, kuna programu nzuri inayofanywa na watu wenye ulemavu kwa ajili ya washiriki kutoka makanisa yanayozunguka eneo la kambi.

 

Nyumba, iliyopatikana kwa fedha kutoka divisheni, katika mji wa mlima uliotembelewa zaidi, Sinaia, ndipo mahali pa kukutania kwa ajili ya makambi madogo, ambapo tunaratibu mikutano ya watu 20-25 wenye ulemavu kutoka mikoa yote ya nchi kwa siku 3 wakati wa msimu wa joto. Kumbukumbu kutoka katika siku hizi adhimu hazisahauliki.

 

Katika shule, chini ya mpango wa Tofauti lakini Sawa, watu wenye ulemavu wanawasilisha uzoefu wao wa ulemavu kwa wanafunzi. Wanapoonyesha uthabiti wao katika mapambano ya kushinda mapungufu, huwavuta na kuwatia moyo wanafunzi kubadilika na kusahihisha mitazamo yao juu ya watu wenye changamoto za kimwili.

 

Ili kushughulikia wale wanaokosa mahitaji ya msingi, tulianzisha Hauko Peke Yako. Ni programu inayotoa chakula, mavazi, usafiri kwa watu wenye matatizo ya kutembea, dawa, na rasilimali nyingine ili kukidhi mahitaji yao na upweke.

 

Kuna watu wenye ulemavu ambao hawajatoka kwenye vyumba vyao kwa miaka mingi. Watu wetu wa kujitolea wenye mioyo mikuu na furaha ya huduma, wamewasaidia kupata familia ya watu wanaokabiliana na changamoto kama hizo. Tumewatoa katika kutengwa kwao ili kuona pwani, milima, nchi za kigeni, na maeneo ya kupendeza macho nchini, mara nyingi kwa mara ya kwanza. Tumeandaa milo ya sherehe kwenye harusi za waliofunga ndoa na kuwatia moyo katika maendeleo ya uwezo wao. Tumewabatiza wale waliotaka kuwa sehemu ya kanisa. Zaidi sana, tumewaonyesha upendo wa Kristo kupitia upendo wa dhati na wa wazi wa watu wa kujitolea.

 

Mipango inaendelea kwa ajili ya “Kituo cha Utunzaji na Ustawishaji” huko Claudia, karibu na Arad, ambacho kitakuwa kimbilio la wale wenye ulemavu ambao hawawezi kujihudumia wenyewe. Mradi huu umeundwa kwa ajili ya wale wenye ulemavu watakaodumu kituoni na pia kwa ajili ya wale watakaokaa kwa muda mfupi tu. Chemchemi za moto, nyumba za kijani zinazoweza kufikiwa kwa ajili ya kilimo asilia, viwanja vya michezo, kanisa dogo kwa ajili ya huduma za kidini, chumba cha kukutania kwa ajili ya tawi la Arad la Inuka na Tembea ambalo lina wanachama zaidi ya 80, na chumba cha tiba ya viungo, vitapatikana kwa ajili ya watu wenye ulemavu nchini na zaidi. Katika kituo hiki tutafanya makambi mengi kwa ajili ya angalau watu 150 ambao watapitia uzoefu wa mtindo bora wa maisha na hali ya kiroho inayoinua.

 

Kama vile Muasisi wa mbinguni alivyofanya kazi katika kuunda familia hii ya Inuka na Utembee, Atapanga utaratibu wa ujenzi wa mahali hapa pa kimbilio kwa utukufu Wake na furaha ya roho nyingi zilizolemewa na changamoto za kimwili.

 

Shauku ya Bwana kutukuza raia wa upendo wake kwa dhifa ya urafiki: “Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete” (Luka 14:21). Ni fursa kwetu kutangaza mwaliko wa Bwana kwa wale wanaotamani urafiki huo wa milele pamoja na Mungu.

Kulingana na Utafiti wa Cerebral Palsy Alliance (CPARF), takribani watu milioni 17 wana aina fulani ya utindio wa ubongo ulimwenguni.1 Katika nchi yangu ya asili Ghana, mwaka 2023, zaidi ya watoto 22,000 kati ya watu milioni 34.1 (0.07% ya idadi ya watu) wanakadiriwa kuishi na utindio wa ubongo.2 Takwimu zinasema kwa uchache au kutosema kabisa kuhusu watu wazima wanaoishi na utindio wa ubongo, lakini mimi ni mmoja wao. Jina langu ni Nii Anyetei Akogyeram, lakini ninafahamika kama Inocki Popo. Babu yangu alinipa jina la Enoch lakini binamu yangu mkubwa alilibadilisha kuwa Inocki na kuongezea jina kipenzi la Popo lililosababisha jina la utani: Inocki Popo.

 

Nilizaliwa Accra, Ghana, mnamo Machi 8, 1990. Wakati wa juma la kwanza baada ya kuzaliwa kwangu, wazazi wangu waligundua kwamba ngozi yangu na sehemu nyeupe ya macho yangu ilikuwa ya njanonjano na walishuku kuwa nina homa ya manjano (hali inayotokea ikiwa kuna bilirubini nyingi katika damu ya mtoto). Kama tiba, waliniweka chini ili kuota jua la asubuhi kwa siku kadhaa. Spektra ya mwanga wa buluu inayopatikana katika mwanga wa jua huvunja kwa urahisi bilirubini nyingi ya ziada ili kuruhusu mwili kuiondoa. Hali yangu iliposhindwa kuwa nzuri, walinipeleka kwa haraka katika Hospitali ya Mafunzo ya Korle Bu, ambapo madaktari walibadilisha damu mbaya katika mwili wangu na damu nzuri kwa njia ya kupewa damu nyingine. Baada ya hayo, waliniweka chini ya miali ya ultraviolet.

 

Miezi mitatu hadi minne baadaye, wazazi wangu waligundua, kwa huzuni, kuwa maendeleo yangu yalikuwa polepole kuliko kawaida. Walinipeleka tena hospitalini lakini daktari aliyenipima aliwahakikishia kuwa hakukuwa na shida.

 

 

KUGUNDUA UTINDIO WA UBONGO

Licha ya kugundua mitetemo na kutoa mate kila mara, madaktari hawakuweza kusema shida yangu ilikuwa ni nini. Hospitalini, nilijifunza, pakawa nyumbani kwangu kwa pili kwa sababu kila mara nilipokuwa na joto lililozidi, waliharakisha kunipeleka huko. Kwa muda mfupi nilifanyiwa mazoezi ya tiba ya mwili. Kwa sababu ya kutoa mate, daktari wangu alinipa kitambaa ambacho nilivaa kwenye mkono wangu wa kushoto na kukitumia kufuta mate wakati yalipotoka. Aliandika maelezo ya dawa ya malaria iliyoitwa Camoquin ambayo familia yangu iliipa jina la utani Jumapili, siku ya kutibu joto la mwili.

 

Nikiwa na umri wa miaka 24, niliamua kujitahidi kujua shida yangu ilikuwa ni nini na nilitumia muda mrefu mtandaoni kutafuta taarifa kuhusu hali yangu. Hatimaye, niligundua kwamba nilikuwa nikipambana na ugonjwa uitwao utindio wa ubongo.

 

Utindio wa ubongo, kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Centers for Disease Control and Prevention [CDC]), “ni kundi la magonjwa ambayo huathiri uwezo wa mtu kusogea, kudumisha usawa na mkao.” Ni ulemavu wa mwili ambao mara nyingi hutokea wakati wa utoto. Utafiti wa CDC unaonyesha kwamba kuna kesi 1 hadi 4 za CP kwa kila wazaliwa hai 1,000. Hata hivyo, nchini Ghana, kesi za CP ni nyingi zaidi, zikiathiri mmoja kwa kila wazaliwa hai 300.3 Kinachozidisha tatizo nchini ni fursa ndogo za matibabu na usimamizi wa kesi.

 

Nilikuwa na utoto mgumu uliosababisha hali yangu kufanyiwa mzaha na kuonewa. Wanafunzi wenzangu walinitania na mara nyingi waliniita kijana mwenye mate. Hawakucheza nami kwa kuhofia kuwa hali yangu ilikuwa ya kuambukiza.

 

Ili kuendeleza busara na kuvumilia uonevu wao, niliamua kutowajali. Kulikuwa na nyakati, hata hivyo, ambapo sikuvumilia uonevu wao wa mara kwa mara na nikajifunza kupambana. Mwishowe, mashambulizi yalipungua na nilikuwa na muda wa kuzingatia masomo yangu.

 

 

KUSHUGHULIKIA UTINDIO WA UBONGO

Kanisani, nilijenga uhusiano mzuri katika madarasa yangu ya Shule ya Sabato. Baba yangu alikuwa mratibu wa huduma za watoto na msaidizi mkuu wa Shule ya Sabato ya watoto. Watoto wengi walikuwa rafiki zangu na walimu wengine walikuwa kwa kweli wanafamilia yangu—shangazi na wajomba. Nilipata fursa ya kushiriki katika shughuli zote—kuimba na kukariri aya za Biblia wakati wa programu za Sabato ya 13.

 

Katika Klabu ya Watafutanjia, baba yangu alikuwa mkurugenzi na mama yangu alikuwa mwalimu hivyo walikuwa na uhakika wa kunijumuisha katika mipango yote. Nilikwenda kambi, kupiga mbizi, kushuka kwa kamba, na kupanda milima. Hivi karibuni nilipitia mafunzo na nikavishwa pini ya kuwa Kiongozi Mkuu. Sasa ninafundisha darasa la Watafutanjia katika kanisa langu mahalia.

 

Mafunzo ya Uongozi wa Kiongozi Mkuu ndiyo yaliyonipa wazo la kuanzisha Popo Cerebral Palsy Initiative.

 

Baada ya kuishi na utindio wa ubongo na kujua jinsi inavyoathiri waathiriwa wake na wazazi wao, nilikufanya kuwa utume wangu ili kuleta ufahamu wa CP kwa umma, haswa kwa wazazi na walezi ambao wanabeba mzigo wa hali hiyo. Pia nilifikiria kwamba ikiwa walimu na wanafunzi wangeelewa hali hiyo wangeweza kuwa na huruma zaidi wanaposhughulika na watu wenye CP.

 

Mnamo Oktoba 2017, nilianzisha Popo Cerebral Palsy Initiative, asasi isiyo ya kuingiza faida. Malengo yangu yalikuwa kuhamasisha wazazi (hasa akina mama wenye watoto wenye CP); kuelimisha umma juu ya hali hiyo; na kusaidia familia zinazoishi na hali hiyo. Maono yangu ni kujenga jamii isiyo na ubaguzi inayokubali na kuheshimu haki za binadamu za msingi za watu wote, ikiwa ni pamoja na watu wenye CP na kutoa fursa sawa kwa watu wote.

 

Familia yangu na marafiki wachache walinishauri kukuza mpango huo kwenye mitandao ya kijamii na kunipa fedha za kuanzia ambazo zilihitajika sana ili kunisaidia kufanikisha ndoto yangu. Nilikuwa na bahati ya kuwa na watu ambao wanashiriki maono yangu.4

 

Ninaona shirika langu lisilo la kuingiza faida kama sehemu ya kushiriki katika utume wa kanisa. Sisi pia tunatazama ulemavu na hasara kupitia lenzi inayobadilisha ya uwezeshaji. Tunaamini katika kile ambacho watu binafsi wanaweza kufanya na wanachoweza kuwa kwa sababu ya neema ya Mungu. Kiini cha kazi yetu ni kupigania kutambuliwa kwa hadhi na heshima kwa kila mtu ili vipaji vyao visivyotambuliwa viweze kuwa njia kwa ajili ya injili. Tunafanya kazi kwa ukaribu na konferensi yetu mahalia kuendeleza mipango inayoshughulikia hali za watu wenye utindio wa ubongo.

Kama Waadventista wa Sabato, moja ya imani yetu muhimu ni ile ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Hakika, ni tumaini “linalowaka ndani ya mioyo yetu.” Na hatuko peke yetu. Ujio wa Kristo umekuwa kilele cha tumaini kwa waumini wote tangu nyakati za kale.

 

Katika kuelezea tukio hilo takatifu, nabii Isaya aliandika, “Katika siku hiyo watasema, ‘Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA; tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake’ ” (Isaya 25:9). Katika Zaburi 50:3 tunasoma, “Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, moto hula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.”

 

Alipokuwa duniani, Yesu aliwaambia wanafunzi Wake, “maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” (Yohana 14:2, 3). Anarudia kutoa ahadi hii kwa kusisistiza katika Ufunuo 22, akisema katika aya ya 7: “Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki” (Ufunuo 22:7); aya ya 12: “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo;” na katika aya ya 20: “Naam; naja upesi.”

 

 

HIYO “UPESI” NI UPESI KIVIPI?

Lakini hiyo “upesi” ni upesi kivipi? Kwa mtazamo wetu wa kibinadamu, hasa katika ulimwengu wa kiteknolojia wa leo, kitu chochote kisicho cha papo hapo ni cha polepole.

 

Waadventista wamekuwa wakihubiri habari ya ujio wa pili wa Kristo kwa miaka 180—ambayo inaweza kuonekana kama milele kwa baadhi. Kwa kuvunjika moyo, baadhi ya Waadventista wamepoteza ufahamu wao wa uharaka wa ujio wa pili wa Kristo, ambao unapaswa kupenya katika kila nyanja ya maisha ya Mwadventista wa Sabato.

 

Hili halipaswi kutushangaza, hata hivyo. Tunasoma katika 2 Petro 3:3-7: “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki,wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, ‘Iko wapi ile ahadi ya kuja kwake? Kwa maana tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.’ ”

 

Petro anasema kwamba hao wenye dhihaka “kwa makusudi wanasahau” kwamba Mungu aliumba mbingu na nchi na kwamba kulikuwa na gharika duniani. Sasa anaonya kwamba siku moja vitu vyote vitateketezwa kwa moto.

 

Aya inaendelea, ikitoa mafundisho ya muhimu na faraja kwa wale waaminio:

“. . . Lakini wapenzi, msilisahau jambo hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu, ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (aya ya 8, 9).

 

 

“KUONEKANA KATIKA AMANI”

Aya hii inatusihi, maadamu dunia na vitu vyote vilivyomo vitaharibiwa, kufikiria kuwa ni watu wa aina gani tunapaswa kuwa “katika mwenendo mtakatifu na utauwa, tukingojea na kuhimiza kuja kwa siku ya Mungu. . .  Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo haya, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake” (aya za 11-14).

Ni wito tulionao, kukaa karibu na Bwana na kumruhusu atuongoze huku tukitazamia kwa hamu kuja Kwake.

 

Kitabu cha Waebrania kinatuhimiza: “. . . msitupe ujasiri wenu kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sasa hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu” (Waebrania 10:35-39).

 

Rafiki, Neno la Mungu linazungumza nasi leo. Usiruhusu mtu yeyote kukunyang’anya tumaini lako katika kurudi kwa Yesu Kristo haraka. Yeye anakuja upesi!

HALISI, BINAFSI, WAZI

Imani ya Msingi #25 ya Waadventista wa Sabato inasema:

“Ujio wa pili wa Kristo ni tumaini lenye Baraka kwa kanisa, kilele cha kuvutia cha injili. Ujio wa Mwokozi utakuwa halisi, wa kimwili, na wa ulimwengu mzima. Atakaporudi, wafu wenye haki watafufuliwa, na watatukuzwa pamoja na wenye haki walio hai na kupelekwa mbinguni, lakini wasio haki watakufa. Utimilifu wa karibu vipengele vyote vya unabii, pamoja na hali ya sasa ya ulimwengu, vinaonyesha kuwa ujio wa Kristo uko karibu. Wakati wa tukio hilo haujadhihirishwa, na kwa hiyo tunaaswa kuwa tayari muda wote.1

 

 

HAKUNA KESHO ILIYOAHIDIWA

Ndani ya mwaka uliopita, hapa katika makao makuu ya Waadventista wa Sabato Silver Spring, Maryland, tumefiwa na viongozi wakubwa wawili—Maurice Valentine, makamu mwenyekiti wa Konferensi Kuu na Bi. Heather-Dawn Small, mkurugenzi wa Huduma za Wanawake kwa kanisa ulimwenguni. Vifo vyote vilikuja haraka sana; yaani ghafla.

 

Rafiki, wakati ni mfupi—hakuna yeyote kati yetu aliyeahidiwa kesho, au hata saa zilizobakia katika siku ya leo. Tuna muda huu tu, sasa hivi. Je, uko tayari kwa ujio wa Yesu? Iwe tunaishi au tunapumzika katika kaburi, tutamwona hivi karibuni.

 

Hali ya sasa ya uharibifu wa dunia inapaswa kutuamsha kuona haja ya umuhimu wa kuwa tayari na kutangaza ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14 kwa kutarajia ujio wa Kristo hivi karibuni.

 

 

MUNGU ANATUTEGEMEA

Mfano wa kuvutia unatuambia, “Katika saa hizi za mwisho za rehema . . . , ambapo hivi karibuni hatima ya umilele wa kila nafsi itakatwa, Bwana wa mbingu na ardhi anatazamia kanisa Lake kuamka na kutenda kuliko wakati mwingine wowote. Wale ambao wamewekwa huru katika Kristo kupitia maarifa ya ile kweli yenye thamani, Bwana Yesu anawachukulia kuwa ni wateule Wake, waliofadhiliwa zaidi ya watu wengine wote juu ya uso wa dunia; naye anategemea watangaze sifa zake Yeye aliyewaita watoke gizani waingie katika nuru ya ajabu. Baraka ambazo zimetolewa kwa wingi sana zinapaswa kuwasilishwa kwa wengine. Habari njema ya wokovu inapaswa kwenda kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa.

Katika maono ya manabii wa kale Bwana wa utukufu aliwakilishwa kama mtoa nuru maalum kwa kanisa Lake katika siku za giza na za kutokuamini kabla ya kuja Kwake mara ya pili. Kama Jua la Haki, angepambazuka kwa kanisa Lake, ‘lenye kuponya katika mbawa Zake.’. . . Na kutoka kwa kila mfuasi wa kweli ilipaswa kueneza ushawishi wa maisha, ujasiri, usaidizi na uponyaji wa kweli.”2

 

Ndugu zangu wapendwa, tunaishi katika mwisho wa nyakati. Hebu tuwe karibu na Bwana, tukimruhusu Roho Mtakatifu kuyajaza maisha yetu tumaini na ujasiri wa kushiriki ujumbe wa ujio wa Kristo hivi karibuni kwa ulimwengu!

“Mungu hatasikiliza maombi ya watu wake wakati yatima, wasio na baba, viwete, vipofu, na wagonjwa hawatunzwi kati yao.”

 

—Testimonies for the Church [Mountain View, Calif.: Pacific Press Pub. Assn., 1948], vol. 3, uk. 518

“Unapowasaidia masikini, kuwahurumia wale wanaoteseka na kuonewa, na kuwa rafiki wa yatima, unajiweka mwenyewe katika uhusiano wa karibu na Yesu.”

 

—Testimonies, vol. 2, p. 25

“Wajane na wasiojiweza wapo kanisani ili baraka kwa Kanisa zionekane. Ni sehemu ya njia ambayo Mungu amechagua kukuza tabia ya kweli ya wafuasi wanaoshuhudiwa na Kristo na kuwaita kuonyesha sifa za thamani za tabia iliyoonyeshwa na Mkombozi wetu mwenye huruma.”

 

—Testimonies, vol. 1, p. 273

“Wale wenye uwezo wanapaswa kushiriki kwa uadilifu, sehemu ya ukarimu katika mpango wao na ndugu zao masikini, na pia wanapaswa kuwapa ushauri mzuri, na kisha wawaache ili kuendelea kupambana na vita ya maisha. Lakini nilionyeshwa kwamba jukumu kubwa zaidi linakaa juu ya kanisa kuwa na huduma ya pekee kwa wajane walio maskini, yatima, na wasiojiweza.”

 

—Testimonies, vol. 1, p. 274

“Lakini kulikuwa na hitaji thabiti la kuwajali wajane, yatima, na wanyonge katika kundi. Licha ya shauku fulani kwa ajili ya kazi kwa ujumla, kulikuwa na shauku ndogo dhahiri kwa familia zao tu. Kwa imani ndogo sana walikuwa wanakufa kifo cha kiroho.”

 

—Testimonies, vol. 2, p. 19

 

WAJIBU WA KANISA

“Watoto yatima wamewekwa mikononi mwa kanisa, na Kristo anawaambia wafuasi wake: Wachukueni watoto hawa maskini, muwalee kwa ajili yangu, nanyi mtapokea ujira wenu. Nimeona ubinafsi mwingi ulioonyeshwa katika mambo haya. Isipokuwa kuna ushahidi maalumu kwamba wao wenyewe wanapaswa kufaidika kwa kuwachukua katika familia zao wale wanaohitaji makazi, wengine hugeuka na kujibu: Hapana. Hawaonekani kujua au kujali kwamba watu wa namna hiyo wameokolewa au wamepotea. Kwa hivyo, wanafikiri, haiwahusu. Pamoja na Kaini wanasema: “Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” Hawako tayari kuingia katika taabu au kujitoa kwa aina yoyote kwa ajili ya yatima, na kwa kutojali wanawaweka mikononi mwa ulimwengu, ambao wakati mwingine wako tayari kuwapokea kuliko hawa wanaodaiwa kuwa Wakristo. Katika siku ya Mungu maswali yataulizwa kwa wale ambao mbingu iliwapa fursa ya kuokoa. Lakini walitamani kupata udhuru, na wasingejihusisha na kazi nzuri isipokuwa wangefanya jambo hilo kama jambo la faida kwao. Nilionyeshwa kwamba wale wanaozikataa fursa hizi za kutenda mema watasikia kutoka kwa Yesu: “Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.” Tafadhali soma Isaya 58: [fungu la 5-11].”

 

—The Adventist Home [Nashville: Southern Pub. Assn., 1952], kur. 167, 168 [mkolezo umetolewa]

“Kazi ya kuwaokoa wasio na makazi na yatima ni jukumu la kila mtu.”

 

—The Adventist Home, uk. 169 [mkolezo umetolewa]

“Wote wanaodai kuwa na baba mbinguni, ambao wanatumaini atawatunza na hatimaye awapeleke nyumbani alikowaandalia, wanapaswa kuhisi wajibu maalumu uliowekwa juu yao wa kuwa rafiki kwa walio wapweke na baba kwa yatima, kuwasaidia wajane, na kuwa wenye msaada katika dunia hii kwa kuinufaisha jamii ya wanadamu.”

 

—The Adventist Home, uk. 169 [mkolezo umetolewa]

WAFUNGULIENI MILANGO YATIMA NA WAPWEKE

“Ilimradi tu iko ndani ya uwezo wako, fanya maskani kwa ajili ya wasio na makazi. Ruhusu kila mtu awe tayari kuchukua jukumu katika kusaidia kuendeleza kazi hii. Bwana alimwambia Petro: “Lisha kondoo zangu.” Agizo hili ni letu, na kwa kufungua milango ya nyumba zetu kwa yatima tunasaidia katika utimilifu wake. Hebu msimruhusu Yesu asikitishwe ndani yenu.”

 

—The Adventist Home, uk. 170 [mkolezo umetolewa]

“Wale wanaowaonea huruma wenye taabu, vipofu, viwete, wanaoteseka, wajane, yatima, na wahitaji, Kristo anawaonyesha kama washika amri, watakaorithi uzima wa milele. . . . Kristo anatazama matendo yote ya huruma, wema, na fikira zinazozingatia walio na taabu, kipofu, kiwete, wagonjwa, mjane, na yatima, kama alivyofanya mwenyewe; Na matendo haya yamehifadhiwa kwenye kumbukumbu za mbinguni na watapewa ujira. Kwa upande mwingine, kumbukumbu itaandikwa katika kitabu dhidi ya wale ambao wanaonyesha kutokujali kwa kuhani na Mlawi kwa wale wanaoteseka, na wale ambao huchukua fursa ya matatizo ya wengine na kuongeza mateso yao ili kujinufaisha wao wenyewe. Kwa hakika Mungu atalipa kila tendo la udhalimu, na kila tendo la kutojali na kupuuza kwa walioteseka kati yetu. Kila mtu atalipwa kulingana na kazi aliyoifanya.”

 

—Testimonies, vol. 3, kur. 512, 513 [mkolezo umetolewa]

“Kuna yatima wanaoweza kutunzwa; lakini wengi hawatajaribu kufanya kazi kama hiyo; Kwa maana inajumuisha kazi zaidi kuliko wanavyoshughulika kufanya, wakiwaacha na muda kidogo wa kujifurahisha. Lakini wakati Mfalme atakapofanya uchunguzi, hawa wavivu, wasiostahili, roho hizi za ubinafsi sasa zitajifunza kwamba mbinguni ni kwa wale ambao wamekuwa watendakazi, wale waliojikana nafsi kwa ajili ya Kristo. Hakuna zawadi zilizoandaliwa kwa ajili ya wale ambao kamwe hawajawahi kufanya huduma maalumu katika kujipenda na kujijali wenyewe. Adhabu ya kutisha ambayo Mfalme aliwaogofya wale waliokuwa upande wa mkono wake wa kushoto, katika jambo hili, sio kwa sababu ya makosa yao makubwa. Hawahukumiwi kwa matendo ambayo walifanya, bali kwa yale ambayo hawakufanya. Hawakufanya mambo ambayo mbingu iliwapa kufanya. Walijifurahisha wenyewe, na wanaweza kuchukua sehemu yao kwa vile walivyofanya.”

 

—Adventist Review and Sabbath Herald, Agosti 16, 1881

“Kuna yatima ambao Kristo amewaagiza wafuasi wake kupokea kama jukumu kutoka kwa Mungu. Mara nyingi huachwa kwa kupuuzwa. Wanaweza kuwa wachafu, wabaya, na kuonekana kutokufaa; lakini bado ni mali ya Mungu. Wamenunuliwa kwa thamani, na ni wa thamani machoni pake kama jinsi tulivyo. Ni washiriki wa familia kubwa ya Mungu, na Wakristo kama mawakala wake wanavyowajibika kwa ajili yao. ‘Roho zao,’ anasema, ‘nitazitaka mikononi mwenu.’ ”

 

—Christ’s Object Lessons [Washington, D.C.: Review and Herald Pub. Assn., 1900, 1941], kur. 386, 387

Carl Christian Hansen, alifanya kazi muhimu katika miaka ya mwanzo ya kanisa la Waadventista wa Sabato huko Denmaki na kutoa muda wake, nguvu na mali ili kuwezesha chanzo alichokipenda.*

 

 

MAISHA YA MWANZO

Carl alizaliwa katika shamba dogo huko Geraa, Denmaki, mwaka 1849, Aprili 27. Miaka saba hadi 14, alisoma shule ya msingi katika majira ya baridi, na katika majira ya kuchipua na majira ya moto alifanya kazi na kaka yake kama mvulana mchunga kondoo ili kusaidia familia yao kubwa. Carl alipokuwa na miaka 14, baba yake aliandaa uanagenzi wake pamoja na mtia rangi katika mji wa Aalborg na baadaye alimsaidia kuanzisha biashara yake ya kutia rangi karibu na nyumbani alipolelewa.

 

Carl alikulia katika jamii ya Kilutheri. Wabaptisti na Wamethodisti walifikiriwa kuwa wapingaji. Mama na dada yake walikuwa Wamethodisti, wakati ambapo baba yake alionekana kuchukuliana na waumini wote. Carl hakuwa na dini mahususi aliyoisadiki. Badiliko lilitokea mwaka 1877 ambapo mchungaji wa Wabaptisti (ambaye baadaye alikuwa Mwadventista), alipomuuzia Biblia. Carl aliamua kuisoma na kuona kama angeweza kuona uhusiano wowote na mitazamo tofauti ya kidini  katika eneo lake.

 

Majira hayo ya joto mke wake, Junia, akawa Mmethodisti. Muda mfupi tu baada ya kuongoka kwake, Carl alisoma Ayubu 28:28, “Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, na kujitenga na uovu ndio ufahamu.” Aya hii iliacha wazo la kina kwake na tangu wakati ule, alipata uzoefu wa msingi wa badiliko la kiroho.

 

 

KUKUTANA NA UJUMBE WA WAADVENTISTA

Carl alikutana na ujumbe wa Marejeo alipotembelea kaya ya Wabaptisti. Mezani, aliona gazeti pamoja na makala kuhusu Danieli 10 vilivyovuta usikivu wake. Alimwuliza mmiliki kujua lilikuwa ni chapisho la namna gani. Mmiliki alijibu kwa kukwepa: “Ninadhani linatoka Marekani, lakini halina thamani yoyote.” Kisha alichukua gazeti na kuliondoa.

 

Carl alikumbuka kuwa gazeti liliitwa Advent Tidende, lililochapwa mwaka 1878, Mei na kuhaririwa na J. G. Matteson. Alikuwa ameshasoma katika gazeti kwamba mmishonari Mwadventista J. G. Matteson ameamsha sehemu kubwa ya dini huko Denmaki na ameanza na harakati za kiasi. Matteson alikuwa akiendesha baadhi ya mikutano huko Alstrup, umbali wa takribani kilomita 50 kutoka alipoishi Carl, lakini, hakupata nafasi ya kuhudhuria.

 

Septemba 1878 mmoja wa wasaidizi wa J. G., Knud Brorson alitembelea mji wa Carl. Knud alimtafuta mchungaji wa Wamethodisti, lakini alipomkosa nyumbani, aliacha kijitabu chenye kurasa 64 The New Testament Sabbath na kuenda zake. Baadaye kidogo, Carl alimtembelea mchungaji wa Wamethodisti kumwambia kwamba mchungaji wa Wabaptisti alikuja nyumbani kwake kumshawishi kuwa imewapasa watu kubatizwa kwa kuzamisha ili kuokolewa.

“Vema,” mchungaji wa Wamethodisti aliitikia: “Wabaptisti wasirejee sana kwenye Biblia kwa sababu wanapaswa kuifuata.”

 

Carl aliuliza, “Je, hawaifuati Biblia?”

Mchungaji wa Wamethodisti akamjibu, “Kama wanataka kuifuata Biblia, wanahitaji kuitunza Sabato na kuitakasa.” Carl alishtuka. Alihojiana na mchungaji kwamba Biblia ilisema kuitunza Sabato. Mchungaji alimjibu, “Haimo. Chukua kijitabu hiki, kisome na utapata kitakachokupa kitu cha kukifiria.” Kijitabu kilikuwa ni The New Testament Sabbath na J. G. Matteson.

 

Kwa majuma mawili, Carl na mke wake walikuwa wakizama kabisa katika kukisoma  kijitabu hicho na wakilinganisha na Biblia. Walipokamilisha utafiti wao, walishawishiwa kwa ukweli wa Sabato na Sabato iliyofuata, Carl alifunga duka lake.

 

Majaribu yalianza mara moja. Marafiki, wakiwemo mchungaji wa Wamethodisti, walimdhihaki yeye na mkewe na kuwaita Wayahudi. Mara kadhaa imani yake ilisita na alihofu kwamba amefanya kosa kubwa. Knud alimjia kama msaada na kumhakikishia kwa kutaja Zaburi 119:105, “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.” Tangu siku hiyo, Carl kamwe hakutilia shaka ukweli.

 

Mei 9, 1879, Carl na Junia walibatizwa. Miezi mitatu baadaye, kanisa la Dronninglund liliundwa na washiriki nane. Kristen Kristensen alikuwa mzee (mchungaji wa zamani wa Wabaptisti ambaye alimuuzia Carl Biblia) na Carl alihudumu kama mweka hazina na karani. Mnamo Mei 30, 1880, Konferensi ya Denmaki (konferensi ya kwanza ya Waadventista nje ya Amerika Kaskazini) iliundwa na makanisa saba. J. G. Matteson alikuwa mwenyekiti, Carl alikuwa katibu na J. P. Madsen alikuwa mhazini.

 

 

KUFANYA KAZI KANISANI

Wakati huo, kulikuwa hakuna mahali nchini Denmaki ambapo vitabu vya Waadventista vingeweza kupatikana. Katika kikao cha pili cha konferensi mwezi Septemba 1881, hatua za kwanza zilichukuliwa kuanzisha kazi ya uchapishaji. Viongozi wa kanisa walimweka Carl kuwa mwanzilishi wa nyumba ya uchapishaji mahalia. Alipata leseni kwa ajili ya shughuli hiyo na alikuwa na jukumu la kuzalisha na kusambaza vitabu kwa miaka minne.

Mwaka 1883 kanisa la Dronninglund liliona umuhimu wa elimu ya Kikristo kwa watoto wao. Carl alikusanya watoto 10 na kuomba idhini ya kufungua shule kwa Wizara ya Elimu. Carl aliandika katika tawasifu yake: “Kazi ilifanikiwa kwa ridhaa ya kila mtu na kulikuwa na uhusiano mzuri na wa upole kati yangu na watoto. Nilikuwa na furaha kubwa katika miaka iliyofuata, kuwa walitembea katika njia ya Bwana na kusimama hadi leo kama washiriki wa kanisa la Mungu.” Shule hiyo ilikuwa shule ya kwanza ya Waadventista barani Ulaya.

 

Wakati Carl alikuwa na umri wa miaka 37, alipewa leseni ya mchungaji na alifanya kazi huko Østervraa kwa mwaka mmoja. Mwisho wa mihadhara yake 16 ya Biblia, E. G. Olsen alikuja na kufanya mfululizo mwingine wa mikutano nane katika siku tano. Ubatizo ulifuata, na kanisa jipya lilianzishwa.

 

Mwaka wa 1888, Carl na familia yake walihamia Odense, ambapo aliitwa kuwa mkurugenzi wa uchapishaji. Aliwasimamia watendakazi wanne, vijana, ambao walikuwa wakiishi nyumbani kwake. Miaka mitatu baadaye, Carl alitolewa kutoka katika jukumu lake la kusimamia kazi ya elimu na kurudi kufanya kazi ya Biblia na uinjilisti. Katika mkutano wa kila mwaka wa Konferensi ya Denmaki huko Copenhagen mnamo 1894, Carl aliwekewa mikono pamoja na wengine wawili. Uwekwaji wakfu huo ulifanywa na mwenyekiti wa konferensi, L. Johnson, na S. N. Haskell na Uriah Smith kutoka Konferensi Kuu.

 

Mnamo mwaka 1897, orodha ya bidhaa kwa ajili ya hospitali ilipelekwa hadi kampasi ya shule ya Frydenstrand huko Frederikshavn na Hospitali ya Frydenstrand ilifunguliwa kama hospitali ya kwanza ya Waadventista nje ya Marekani. Carl alihudumu kama meneja wa biashara wa shule na hospitali hadi zilipohamishiwa kwenda Copenhagen.

 

 

MIAKA YA BAADAYE NA URITHI

Wakati Carl aliacha kuhudumu kama meneja wa biashara mnamo Machi 1905, alinunua duka la vyakula vya kiafya na kufungua “Sana,” ambapo aliwekeza nguvu zake zote katika kukuza mtindo wa maisha ya kiafya. Mwaka 1916, alihamisha umiliki kwa binti yake Kristine ili “nitoe wakati wangu wote kwa utumishi wa Bwana,” kama alivyoeleza. Mara nyingi aliwatembelea washiriki, alifanya mikutano nyumbani, alipenda kushiriki katika kampeni za kukusanya michango, alihubiri na alifanya kazi kama mzee katika makanisa mawili madogo nje ya Copenhagen. Carl alifariki mnamo mwaka 1932.

Waadventista wanaamini kwamba Biblia haifundishi asili ya roho isiyokufa na wanakiri kwamba binadamu ni muunganiko usioweza kugawanyika wa maisha katika umbo la mwili. Hivyo, kutokufa ni zawadi tutakayopewa na Mungu mwisho wa wakati isiyoweza kutenganishwa na kufufuka kwa mwili (1 Kor. 15:50-55). Ingawa mwanzoni mwa enzi ya Kikristo kulikuwa na tafsiri tofauti za roho ya binadamu, kanisa la Kikristo lilikubali mtazamo kwamba roho kwa asili huishi milele, ikiishi katika mwili ambamo inaachiliwa kutoka wakati mwili unapokufa.

 

 

1. ROHO NA HALI YA BINADAMU

Hali ya asili ya kutokufa kwa roho kunadai kwamba roho haiharibiki na hivyo hakuna nguvu ya nje, wala hata nguvu ya Mungu inayoweza kuiangamiza (angalau, Mungu anaonekana kutokuwa tayari kufanya hivyo). Hitimisho dhahiri ni kwamba dhambi haijatishia kuwepo kwa roho. Kitu fulani ndani yetu kimeepuka jeraha la kufisha la dhambi. Hata hivyo, Biblia inafundisha kwamba, dhambi imedhuru kabisa mtu kwa ujumla wake—maisha ya ndani pamoja na kiroho, kimwili na kijamii—ikimwacha mtu katika hitaji la wokovu (Mwa. 3:8-13; Rum. 8:6-7; 6:23). Maandiko yanafundisha kwamba, roho inayotenda dhambi ndiyo itakayokufa (Eze. 18:4; linganisha na Rum. 1:32). Chaguo pekee ni kuwa kiumbe kipya kupitia kafara ya Kristo ya kuokoa (Yn. 3:7; 2 Kor. 5:17).

 

 

2. ROHO NA WOKOVU

Imani kwamba uwepo wa binadamu kamwe haukuwa katika hatari inapunguza kina cha kafara ya upendo wa Kristo. Hakujitoa maisha Yake ili kuokoa roho kwa sababu roho haihitaji kuokolewa—yaani, kupewa uzima wa milele! Wale wanaoamini katika kutokufa kwa roho bila shaka wanatoa hoja kwamba ni eneo ambalo roho isiyoweza kufa itaendelea kuwepo ndilo lilikuwa katika hatari lakini si roho yenyewe. Roho, wanatoa hoja, inahitaji kurudi kwenye eneo la Mungu kupitia kazi ya upatanisho ya Kristo ili kuepuka mahali pengine pa pili pa maisha yenye mateso. Wamebadilisha uharibifu ambao dhambi na uasi vilisababisha kwa asili ya binadamu, na wakati huo huo kupunguza ukubwa wa kafara ya Kristo—Hakufa ili kutupa uzima bali ili kufanya uzima wetu wa asili uwe wenye furaha. Ukweli ni kwamba, kafara Yake ilihusisha kushuka hadi kwenye eneo la mauti ili kuturudishia uzima wa milele tulioupoteza (Marko 10:45; Yn. 3:16; 10:28; Rum. 6:23). Lazima tukiri kwamba, hakuna kitu kilichoponyoka nguvu ya kifo cha dhambi na kwamba, ili kutuokoa kafara kubwa ilihitajika (2 Kor. 8:9; Flp. 2:7; Mt. 27:43). Wazo la roho isiyoweza kufa linaharibu utukufu wa upendo wa kusulubiwa kwa Mungu.

 

 

3. ROHO NA HUKUMU

Mafundisho ya asili ya roho kutokufa yanapotosha tabia ya upendo ya Mungu kama ilivyoonekana kwenye msalaba kwa kubadilisha kifo cha milele kama kuteketezwa milele kwa roho ya waovu kuzimu. Hata ni chungu kufikiria kwamba Kristo anawachoma watu kwa makusudi milele kama adhabu kwa kuishi maisha mafupi yenye dhambi kwenye sayari hii. Hili ni moja ya janga kubwa kabisa la mafundisho ya imani katika historia ya Ukristo na inaonekana wazi ni matokeo ya kukubali imani katika kutokufa kwa roho. Mungu si Bwana mkatili kama huyo, kwa maana yeye ni upendo (1 Yn. 4:8; Ufu. 21:3-4). Kulingana na Biblia, waovu wataangamia milele (linganisha, Mal. 4:1; Zab. 37:10; 145:20).

Ulimwenguni kote, saratani ni chanzo kikuu cha kifo baada ya ugonjwa wa moyo na mishipa (shambulio la moyo na kiharusi). Mwaka 2020, saratani ilisababisha vifo vya takribani watu milioni 10. Saratani za matiti, mapafu, utumbo mpana na mjiko na tezi dume ndizo zinazojulikana zaidi. Takribani watoto 400,000 hupata saratani kila mwaka.

 

Hizi ni takwimu na ukweli wa kutisha. Hata hivyo, kuna habari njema. Masomo mbalimbali ya Afya ya Waadventista yameonyesha faida fulani kwa wanaokula vyakula vya mboga-mboga. Walaji wa mboga, mayai na maziwa walifanya vizuri zaidi kwenye saratani ya utumbo (utumbo mpana na mjiko) kuliko walaji mboga pekee (wasiotumia bidhaa za wanyama); hii labda inahusiana na kalsiamu inayopatikana kwenye bidhaa za maziwa. Walaji mboga pekee walifanya vyema zaidi kuliko walaji mboga wengine kwa saratani ya matiti na tezi dume, labda ikihusiana na kutokuwepo kwa maziwa. Kwa ujumla, wale wanaofuata lishe ya mboga ya aina fulani walikuwa na matokeo bora ya saratani na maisha marefu.

 

Sababu hatarishi za saratani ni pamoja na:

  • Matumizi ya tumbaku
  • Unene kupita kiasi (uwiano wa juu wa mwili)
  • Unywaji wa pombe
  • Utumiaji wa kiwango cha chini cha matunda na mboga
  • Ukosefu wa shughuli za kimwili na mazoezi
  • Hewa chafu
  • Mwanga wa jua kupita kiasi na mitambo ya kubadilisha ngozi (saratani ya ngozi pamoja na melanomas)
  • Maambukizi ya muda mrefu kama vile saratani ya shingo ya kizazi kutoka katika virusi vya human papilloma (HPV), na saratani ya ini kutokana na maambukizi ya homa ya ini (haya yanachangia asilimia 30 ya saratani katika nchi za kipato cha chini)
  • Magonjwa ya kurithi kama vile ugonjwa wa Lynch, au saratani ya utumbo mpana, pia inajulikana kama ugonjwa wa saratani ya colorectal hereditary nonpolyposis.

Mzigo wa saratani kwa ujumla unaweza kupunguzwa kwa asilimia 30 hadi 50 kwa kudhamiria kuepuka vyanzo vya hatari. Epuka matumizi ya tumbaku na pombe; hakuna kiwango salama cha matumizi kwa mojawapo ya visababishi hivi vya saratani. Jitahidi kudumisha uzito wa kawaida wa mwili. Kula kwa afya, ukijumuisha sehemu tano hadi saba za matunda na mboga kila siku na lishe bora ya mboga. Fanya mazoezi mara kwa mara na ufurahie shughuli za mwili kila siku. Epuka mionzi ya ziada ya miali kutokana na matumizi ya mitambo ya kubadilisha rangi ya ngozi; tumia mafuta yanayofaa unapokuwa katika miali ya jua moja kwa moja. Matumizi rasmi ya chanjo ya HPV na hepatitis husaidia kuzuia.

 

Matibabu sahihi ya saratani yanaweza kupunguzwa zaidi na utambuzi wa mapema wa saratani. Inapotambuliwa na kugunduliwa mapema, nafasi za matibabu yenye mafanikio na kupona huboreshwa zaidi. Ni muhimu kutafuta ushauri wa kitaalamu wakati mtu anapotambua dalili mpya kama vile uvimbe, damu kwenye kinyesi au mkojo, au kutokwa na uchafu usio wa kawaida/kutokwa damu kwenye ngozi, matiti au mfumo wa uzazi.

 

Vipimo vya uchunguzi vinavyosaidia ni pamoja na:

  • Papanicolaou (Pap) vipimo vya saratani ya shingo ya kizazi
  • Mammography kwa ajili ya saratani ya matiti
  • Colonoscopy
  • Uchunguzi wa kidijitali wa puru kwa wanaume ili kugundua saratani ya tezi dume na vipimo vya damu kama inavyoshauriwa.
  • Uchunguzi wa mara kwa mara wa afya ya kinywa/meno

 

Kinga nyingi zilizoorodheshwa katika makala hii fupi ni pamoja na mapendekezo ya kuhifadhi na kuweka katika vitendo ujumbe wa afya wa Waadventista. Hata hivyo, tunaishi katika ulimwengu ulioharibika. Hadi Yesu atakaporudi, tutakabiliana na kifo ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kufa kutokana na saratani. Hata hivyo, kwa ujumla tutakuwa tumepata fursa ya maisha bora, huenda hata maisha marefu zaidi, na miaka mingi ya kumtumikia Bwana na kanisa tunalolipenda. Kwa ufupi—inafaa kufuata Ujumbe wa Afya wa Waadventista. Maranatha!

 

Sauti ya Betty ilisikika vizuri na moja kwa moja. “Jim siwezi kuishi pamoja na wewe tena. Unatakiwa kuondoka hapa nyumbani kabla sijatoka kazini leo.”

 

Ilikuwa Ijumaa, vitu havikuwa vikienda sawa kati ya Jim na Betty, wenzi wachanga, familia ya kichungaji ya Waadventista. Betty alikuwa amevunja ndoa na Jim hakuwa ameelewa mbona.

 

“Nilidhani tulikuwa na ndoa ya mfano, yenye uhusiano mzuri” anakumbuka. “Lakini sasa kitu kibaya zaidi ambacho sikuwahi kukidhania kilikuwa kinatokea na wala hata sikujua nilipaswa kufanya nini!”

 

Jim alimpigia simu mchungaji wa hospitali na kumwomba amsaidie kutoa somo badala yake siku iliyofuata, kisha akapanda RV, gari lao la zamani, na kuelekea kusini. Matembezi ya muda mrefu ya Pacific Crest Trail yangemsaidia kutuliza kichwa chake, alitumaini. Kwa vipindi vya usiku alitumia kukaa karibu na reli za matreni. Sabato asubuhi alikuwa kusini ya mbali. Kisha gia ilitoa sauti ya kutisha yenye kukwaruza, kukwama na kuacha.

 

 

KUKWAMA KATIKA MJI MDOGO

Ilichukua muda kidogo, lakini hatimaye gari la kubebea magari nyumba lilivuta lile gari nyumba lake hadi kwenye karakana ya mafundi wa ubadilishaji gia wa eneo hilo ambapo walilichungua haraka na kumpa Jim habari.

 

“Linaweza kurekebishwa, lakini tunafunga saa sita mchana leo kwa hivyo hatutaweza kuanza kufanya kazi mpaka Jumatatu. Mpaka wakati huo, unaweza kufanya kambi hapa katika eneo letu la maegesho.”

 

Hivi sivyo alivyokuwa amepanga kuitumia Sabato.

 

Usiku huo, ghasia za genge zilizuka katika eneo la maegesho, zikilizingira gari nyumba kwa milio ya risasi, kelele, matairi yakipiga kelele, na ving’ora. Kwa kuhofia maisha yake, Jim alitumia muda mwingi wa usiku akiwa amelala sakafuni mwa gari nyumba, akimlilia Mungu kimya kimya.

 

Asubuhi ya Jumapili, Mchungaji Jim aliamka akihisi kwamba anahitaji kuwa kanisani—kanisa lolote. Alianza kutembea na punde chini ya barabara alisikia muziki wa Kikristo ulioimbwa kwa ari kubwa. Ishara mbele ya kanisa ilisema “Ushuhudiaji wa Ushindi.” Alipoingia katika kanisa dogo, mara moja aligundua kwamba watu hawa hawakuwa kama watu waliokuwa wakihudhuria katika kanisa lake kubwa nyumbani. Jinzi na fulana, michoro na kujichoma, kanisa hili lilionekana kulenga waraibu na wanaoishi mitaani. Walikuwa wakiimba kwa sauti kuu, wakimsifu Mungu mwenye upendo na msamaha.

 

Muziki ukipenya moyoni mwake, Jim alianza kulia bila kujizuia. Washiriki walionekana kuimba kwa sauti kubwa iliyofunika sauti ya kilio chake, na Jim alijua kwamba Mungu alimwongoza moja kwa moja mahali alipohitaji kuwa.

 

Wakati ibada ilimalizika, alivuta usikivu wa mwanamke mmoja kwenye kiti mbele yake.

“Niko katika matatizo,” alisema. “Je, Kuna mtu naweza kuzungumza naye?”

“Subiri kidogo tu,” alijibu.

 

Muda mfupi baadaye, shemasi ambaye ni kijana alikuja na kuketi karibu naye. Jim alipoweka wazi kinachomsababisha kulia, mwanaume huyo alisikiliza kwa makini. Jim alipoweka kituo, shemasi alizungumza moja kwa moja kwa moyo wake. “Kuna kitu sijakielewa. Mchungaji wa Kikristo anawezaje kuruhusu ndoa yake kufikia hali mbaya hivyo kiasi kwamba mkewe anapendelea kuishi bila yeye?”

 

Swali lilikuwa la kushangaza. “Huelewi. Yeye ndiye aliyenifukuza nyumbani. Sikua na chaguo.” Shemasi aliendelea. “Huwezi kurekebisha kile ulichokivunja ukiwa hapa. Lazima uende nyumbani.”

 

“Siwezi.”

 

“Lazima.”

 

 

UMOJA WA MAOMBI

Nje, Jim alianza kuzurura mjini. Alitembea, akiwaza, akitafakari kuhusu kile alichokisikia na uzoefu alioupata, akilia machozi njiani.

 

Asubuhi hiyo baadaye, matembezi ya Mchungaji Jim yalimfikisha katika hospitali mahalia. Hewa iliyo yoyozwa katika chumba cha wagonjwa kusubiria ilikuwa yenye kustarehesha. Baada ya kudurusu magazeti machache, aligundua kuna kanisa dogo nje tu ya chumba cha wagonjwa kusubiria. Akaingia, akapiga magoti karibu na kiti kimoja na akaomba, akitafuta amani na maarifa. Baada ya muda wa kuwa peke yake, aliinuka. Alipoanza kuondoka kutoka kanisani, akatambua kuwa kuna jalada la maombi ya kuombea.

 

“Mimi ni mchungaji wa Kikristo,” Jim aliandika kwenye kurasa iliyo wazi. “Mke wangu amenifukuza nyumbani. Tafadhali naomba mniombee.” Kisha akaandika sahihi ya jina lake.

 

Jumatatu asubuhi, makanika walivuta gari nyumba hilo la zamani ndani ya gereji na wakaanza kushughulikia gia.

Jim aliondoka kutembea.

Huku akilia kwa sauti.

Na akitafakari.

 

Akajikuta amerudi tena hospitalini. Hakukuwa na yeyote ndani ya kanisa dogo, lakini aliweza kusikia mchungaji wa hospitali akizungumza na simu katika ofisi ya jirani. Mtu yule alipomaliza kuzungumza na simu, Mchungaji Jim aligonga mlango wa mchungaji wa hospitali.

 

“Karibu ndani!” sauti ya ukarimu ilimkaribisha.

“Niliingia ndani, nikakaa chini na kufuta macho yangu yaliyolowa chepechepe. Nilipoinua macho, niliona sura ya mtu mwenye huruma akinipatia boksi la karatasi laini,” Jim anakumbuka.

 

“Nikusaidie nini?”

 

“Mimi ni Mchungaji Jim,” alianza.

 

“Wewe ni Mchungaji Jim?!” Mchungaji wa hospitali alishangaa.

 

“Ndiyo, mimi ndiye,” Jim aliitikia kwa mkanganyiko.

 

“Kabla hujasema neno lolote, Jim, ninahitaji ujue kitu fulani. Kila mchungaji wa Kikristo katika mji huu anakuombea kwa kukutaja kwa jina katika asubuhi hii. Ujumbe ule uliouandika katika kitabu cha maombi ndani ya kanisa dogo jana, nilishiriki na wachungaji katika maombi ya kila mwezi asubuhi hii! Wote tulikuombea na wanakuombea sasa!”

 

Jim hakuweza kuamini kile alichokuwa anakisikia. Mungu alikuwa ameandaa zawadi ya ajabu kwake.

 

“Huko, katika mji asioufahamu, mbali na nyumbani, wachungaji wote Wakristo walikuwa wakimwomba Mungu kwa niaba yangu. Ni jambo la kushangaza.”

 

Jim na mchungaji wa hospitali walikuwa wakiomba na kuzungumza pamoja. Hatimaye, mchungaji wa hospitali akamwekea mkono begani Mchungaji Jim na kusema, “Jim, unahitaji kurudi nyumbani. Huwezi kutengeneza kile kilichovunjika katika ndoa yako ukiwa hapa!” Jim aliutambua ushauri huo na alijua alipaswa kufanya nini. Lakini alikuwa na hofu kubwa kufuata maneno hayo. Je, ikiwa angepiga simu na Betty akakata?

 

Aliporudi katika gereji ya kutengeneza magari, aliketi katika chumba kidogo cha kungojea, akili yake ikikumbuka polepole maneno tena na tena. “Huwezi kutengeneza kile kilichovunjika ukiwa hapa!” “Nenda Nyumbani Sasa!”

 

Wakati marekebisho ya gari nyumba yalikamilika hatimaye, Jim alipiga simu akitetemeka kwa hofu kwa kanisa lake. Mkewe, Betty, angekuwepo na watoto kwenye mkutano wa kila juma wa klabu ya Watafutanjia.

 

“Ninaweza kuzungumza na Betty tafadhali?” Sauti yake ilisikika kama tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7, moyo wake ukipiga kwa matumaini yaliyojaa hofu.

 

“Halo, mimi ni Betty.”

 

“Halo, mimi ni Jim.”

 

“Jim, unaweza kurudi nyumbani. Niahidi tu tutaenda kwa ajili ya msaada pamoja. Mungu anatutaka tufanye hili, kwa pamoja.”

“Kuna shida gani?” Laray alimwuliza aliyekuwa akikaa naye chumba kimoja, Keishla.

 

Keishla alitazama kutoka kwenye trei ya mkahawa mbele yake. Supu ya mboga na skonzi motomoto za Bi. Sonia kila wakati kilikuwa chakula chake pendwa! Lakini supu ilikuwa inapoa wakati alipokuwa akiiangalia.

 

“Umekuwa kimya na mwenye huzuni asubuhi yote,” Laray alisihi. “Nini kinakusumbua?”

“Sijui Damien yuko wapi,” Keishla alisema kwa kumumunya.

Laray akainua kijiko chake kwenda mdomoni. “Je, ndiye kaka yako mkubwa?”

Keishla alikubali kwa kichwa. “Kaka yangu kipenzi.” Alisukuma kiti chake nyuma na kuanguka chini. Kengele ilipogonga kwa ajili ya madarasa, wasichana walisimama na kuondoa sahani zao na kuzipeleka jikoni.

 

Wasichana wengine wa darasa la saba walipokuwa wakifanya utani kwenye njia za bwalo wakienda kwenye darasa la hesabu, Keishla alijificha kwenye ofisi ya Mchungaji Paul na kuzama kwenye kiti kando ya meza yake. Akimtazama, aliona macho yaliyosononeka, na alijua kuna kitu hakiko sawa.

 

“Je, umekuwa na juma baya?” Mchungaji Paul aliuliza.

Keishla akakubali kwa kichwa.

“Unataka kunieleza kuhusu hilo?” alihamasisha kwa upole.

Kichwa cha Keishla kiliinama chini.

“Sioni namna ya kuacha kumfikiria Damien,” alisema kwa kunong’oneza. Keishla na dada yake mdogo walikuwa wanasoma kwenye Shule ya Holbrook Indian. Wanafunzi wote kutoka darasa la 1 hadi la 12 walikuwa wanaishi katika mabweni ya shule. Ingawa kwa kawaida alikuwa na furaha, hisia za upweke kwa kaka yake zilifanya maisha kuwa magumu kwa Keishla.

 

“Huwezi kumpigia simu au kumtumia barua pepe?” Mchungaji Paul aliuliza.

Keishla alitikisa kichwa chake kwa huzuni. “Hatuna anwani au namba ya simu yake.” Alipangusa mikono yake kwa wasiwasi kwenye suruali yake ya jinzi.

 

Baada ya kutafakari mambo kadhaa, Mchungaji Paul alisema, “Angalia, Keishla, Yesu anajua kabisa mahali ambapo Damien yuko, sivyo?” Macho yake yenye huzuni yalimwangalia. Keishla alikuwa ametoa moyo wake kwa Yesu na kuwa wa kwanza kubatizwa katika familia yake ya Navajo miezi iliyopita. Tangu siku hiyo hakuwahi kupoteza tabasamu lake la kupendeza—mpaka wakati huu.

 

“Kwa nini tusiombe tu na kumwuliza akuambie cha kufanya?” Mchungaji Paul aliuliza. Keishla akakubali kwa kichwa na kuinamisha kichwa kwa ajili ya maombi.

“Mpendwa Mungu, Keishla anamkumbuka sana kaka yake,” Mchungaji Paul aliomba. “Unajua mahali ambapo Damien yupo. Tafadhali msaidie Keishla kumpata.” Mchungaji Paul alitulia kwa muda na kumtazama Keishla. Keishla alimwangalia na mchungaji alimtia moyo kwa kuitikia kwa kichwa.

 

Keishla alifunga macho yake tena. “Mpendwa Yesu, je, unamuona Damien?” Aliomba. “Tafadhali, je, unaweza kumpeleka nyumbani?” Machozi yaliisonga sauti yake. “Nina wasiwasi juu yake. Je, yuko salama? Tusaidie kumpata. Amina.”

 

Mchungaji Paul alisimama. “Twende,” alimwongoza kuelekea mlangoni, "Twende kumwona Bi. Brown.”

 

Kama kawaida, ofisi ya Bi. Brown ilikuwa imezungukwa wanafunzi. Mmoja alihitaji dawa, mwingine alikuwa na fomu ya kujaza na mtoto wa darasa la nne alikuwa na swali ambalo yeye pekee angeweza kulijibu. Kama msajili, makamu mkuu wa shule na mshauri, Bi. Brown alikuwa na shughuli nyingi.

 

Mchungaji Paul alipoeleza hali ya Keishla, Bi. Brown aliwatoa wanafunzi wote na kukaa nao.

 

Kwa msaada wa Mchungaji Paul, Keishla alielezea tatizo lililomfanya ajisikie mwenye huzuni na wasiwasi. Bi. Brown akiwa kimya alisikiliza kisha akauliza maswali kadhaa kwa upole. Polepole, hali ya Keishla ilianza kuwa bora. Hatimaye, waliomba pamoja kwa ajili ya kupata njia ya kumpata Damien. Kulikuwa na ishara ya matumaini kwenye uso wa Keishla alipoondoka kwenda katika kipindi kilichofuata.

 

Mchungaji Paul alikawia kwa muda kwenye ofisi ya Bi. Brown wakijadili njia zinazowezekana za kumpata Damien. Hakika kulikuwa na njia ya kumpa ujumbe kwamba dada yake alikuwa akimtamani kuzungumza naye. Lakini hakuna jibu lililotoka kwa yeyote kati yao.

 

Usiku huo wakati wa kujisomea bwenini, Keishla aliitwa kutoka bwaloni kwenda kwenye ofisi ya mshauri.

 

“Unapigiwa simu,” mshauri alisema huku akimkabidhi simu.

“Ni nani?” Keishla aliuliza.

“Sijui,” alisema.

Keishla alisitasita kwa kuinua mabega na kwa uso wa kushangazwa akasema, “Halo?”

“Keishla? Mimi ni Damien,” sauti ilisema.

Keishla akatoa simu na kuiangalia kwa kutokuamini. “Nani?” alihoji.

“Mimi ni Damien, kaka yako,” sauti ilirudia. “Nimezungumza na mama na alisema nikupigie simu.” Akatulia. “Unaendeleaje?”

Kwa sasa, moyo wa Keishla ulikuwa ukidunda kwa taharuki. “Damien? Damien, kaka yangu?” aliuliza kwa mshangao kwenye simu. “Uko wapi? Kwa nini hujapiga simu mpaka sasa? Sijakuona kwa miaka miwili!” Maneno yake yalitoka kwa kupandiana.

 

Katika taharuki hiyo, mshauri alimwita mdogo wake wa kike, Karina, ofisini. Akitabasamu, Keishla alimkabidhi simu. Akifikiria kuwa angekuwa mama yake, Karina alichukua simu.

“Halo,” Karina alisema.

“Mambo, Karina! Mimi ni Damien.”

“Nani?” Karina aliuliza kwa mshangao. Alimwangalia Keishla ambaye alikuwa ameweka mkono mdomoni mwake akijizuia kucheka. Akisikiliza sauti ya kaka yake, macho ya Karina yalianza kufunguka. Ghafla akapiga yowe ambayo ilisikika kwenye barabara ya bweni. Sasa Keishla alikuwa akicheka na Karina alikuwa analia alipogundua kwamba huyu kweli alikuwa kaka yake, Damien!

 

Ingawa Mchungaji Paul na Bi. Brown hawakuweza kupata mpango wa kumpata Damien, Mungu alikuwa na mpango uliokuwa unaendelea hata walipokuwa wanamwomba.

 

Kwa wakati wa mapumziko ya Shukrani, Damien aliwaalika familia yake yote kwenda alipokuwa huko Phoenix, Arizona. Baada ya miaka miwili mirefu, familia ilikuwa pamoja! Na unaweza kuwa na hakika kwamba sehemu bora ya likizo hiyo kwa Keishla haikuwa chakula kizuri. Ilikuwa jibu la ajabu kwa maombi yake kwa Mungu kumpata Damien. Keishla alijua jinsi gani Daudi alivyohisi alipoandika, “Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu” (Zaburi 55:17).

Mchapishaji

Jarida la Adventist World, jarida la kimataifa la Kanisa la Waadventista wa Sabato. Konferensi Kuu, Divisheni ya Asia Pasifiki ya Waadventista wa Sabato ndio wachapishaji.

 

Mkurugenzi Mtendaji/ Mkurugenzi wa Huduma za Adventist Review

Justin Kim

 

Meneja wa Uchapishaji wa Kimataifa

Hong, Myung Kwan

 

Kamati ya Uratibu ya Jarida la Adventist World

Yo Han Kim (chair), Tae Seung Kim, Hiroshi Yamaji, Myung Kwan Hong, Seong Jun Byun, Dong Jin Lyu

 

Wakurugenzi wenza/ Wakurugenzi, Huduma za Adventist Review

Sikhululekile Daco, John Peckham, Greg Scott

 

Wahariri waliopo Silver Springs, Maryland, Marekani

Enno Müller, Beth Thomas

 

Wahariri waliopo Seoul Korea
Hong, Myung Kwan; Park, Jae Man; Kim, Hyo-Jun

 

Mkurugenzi wa Mambo ya Kidijitali

Gabriel Begle

 

Mkurugenzi wa Muungano wa Mifumo na Uvumbuzi

Daniel Bruneau

 

Meneja wa Shughuli

Merle Poirier

 

Mratibu wa Tathmini ya Uhariri

Marvene Thorpe-Baptiste

 

Wahariri /Washauri wengine

E. Edward Zinke

 

Meneja wa Fedha

Kimberly Brown

 

Mratibu wa Usambazaji

Sharon Tennyson

 

Mratibu wa toleo la Kanda (Adventist World)

Penny Brink

 

Bodi ya Utawala

Yo Han Kim, chair; Justin Kim, secretary; Hong, Myung Kwan; Karnik Doukmetzian; SeongJun Byun; Hiroshi Yamaji; Joel Tompkins; Ray Wahlen; Ex-officio: Paul H. Douglas; Erton Köhler; Ted N. C. Wilson

 

Maelekezo ya Usanifu na Muundo

Types & Symbols

 

Kamati ya Adventist World ya Divisheni ya Afrika Mashariki – Kati:

Blasious Ruguri, Musa Gideon Mitekaro, Tom Ogal, Emanuel Pelote.

 

Tafsiri

Ufunuo Publishing House, South Tanzania Union Conference.

 

Msomaji wa prufu

Lilian Mweresa

 

Usanifu wa toleo la Kiswahili

Daniella Batista, Ashleigh Morton, Digital Publications

 

Uchapishaji wa Kidijitali

Charles Burman, Digital Publications (www.digitalpublications.co.za)

 

Muelekeo wa Sanaa na Ubunifu

Mark Cook, Brett Meliti, Ivan Ruiz-Knott

/Types & Symbols

 

Kwa Waandishi: Tunakaribisha miswada huria. Tuma barua zote kwa uhariri kwa 12501 Old Columbia Pike, Silver Spring, MD 20904-6600, U.S.A. Faksi ya ofisi ya Uhariri ni: (301) 680-6638

 

Waraka pepe: worldeditor@gc.adventist.org

Tovuti: www.adventistworld.org

 

Rejea zote za Biblia zimechukuliwa kutoka kwenye Swahili Union Version Bible Toleo la Chama cha Biblia la mwaka 1952.

 

Jarida la Adventist World linachapishwa kila mwezi na kuchapwa kwa wakati huo huo huko Korea, Brazili, Indonesia, Australia, Ujerumani, Austria, Ajentina, Meksiko, Afrika Kusini, na Marekani.

 

Vol. 20, Na. 4

Swipe left

swipe left To move to the next page

Swipe right

swipe right To move to the previous page
Allow Send-it to use cookies?

Send-it uses cookies to track how you use the application. Find out more about what data we collect and how we use the data in our privacy policy.